Thursday, February 28, 2013

MAKTABA NCHINI ZAPEWA CHANGAOTO



Mkuu wa mkoa wa singida Dr Paseko Kone amezitaja maktaba nchini kuwa mstari wa mbele  katika harakati za kuleta maendeleo nchinikwa kupunguza watu wasiojua kusoma na kuandika

Akihutubia katika warsha ya  maendeleo ya sekta ya maktaba Tanzania iliyofanyika mkoani Singida leo, amesema warsha hiyo inasaidia kujadili mchango wa tasnia ya maktaba katika kuchangia juhudi za serikali za kuleta maendeleo na kuboresha sekta ya elimu na hali ya maisha ya Tanzania.

Dk. Parseko Kone amesema ni wajibu wa kila maktaba pamoja na wakutubi kuhakikisha wanatoa huduma sahihi zinazokidhi mahitaji ya watumiaji katika jamii.
 
Wakutubi kutoka mikoa yote nchini wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Singida, wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa wakutubi nchini ambao umefanyika wiki hii mkoani Singida sambamba na kuchagua viongozi wao wa kitaifa. Picha na Edilitruda Chami

Katika mkutano huo Dr. Kone amewataka wananchi hasa waishio vijijini,  kuondoa dhana potofu waliyojijengea kwamba maktaba ni kwa ajili ya wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani tu, kwani kutonakana na fikra hiyo hata idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika inaongezeka.

Amesema maktaba ni sehemu nzuri kwa watu kupumzika huku wakijisomea vitabu, magazeti na kusoma habari mbali mbali kupitia mitandao ya kompyuta hivyo ni vyema watu  kuwa na nguvu ya kuchemsha bongo kwani akili ikichemka mtu hupata furaha na kuongeza maarifa.

No comments: