Saturday, February 16, 2013

TAARIFA YA HABARI KUTOKA STANDARD RADIO FM- SINGIDA


Source: E

Ed:Im

Date February 16,2013

SINGIDA

Wito umetolewa kwa serikali na jamii kutambua mchango wa vikundi  vinavyochipukia katika jamii  ili kuharakisha maendeleo

Akiongea na rdio standard  mwalimu w akikundi cha saa cha sanaa Gineri Bw.Henry Lyimo amesema  kuwa baadhi ya watu wamekuwa na mtazamo tofauti kuhusu vikundi hivyo  pamoja na kutoonyesha ushirikiano pale unapohitajika.

Aidha amesema jamii ni lazima itambue umuhimu wa vikundi kwani vinasaidia kuelimisha  pamoja na kusaidia jamii kuondokana na kuzurura bila kazi na pengine kusababisha baadhi yao kujiingiza kwenye vitendo viovu.

Aidha ameikumbusha  serikali  kuvipa msaada pindi viapohitaji ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi na kuondokana na umaskini      

 


 

Source: E

Ed:Im

Date February 16,2013

MWANZA

Halmashauri ya wilaya ya magu mkoani mwanza kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi ya wilaya hiyo imefanikiwa kufanya utambuzi wa watu wenye ulemavu wa ngozi albino pamoja na kuwapatia ulinzi kwa kutoa elimu kwa jamii dhidi ya imani potofu kwamba viungo vya albino vinaleta utajiri.

Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Magu, Mwl. Naomi Nko amesema hadi sasa watu wenye ulemavu wa ngozi Albino katika halmashauri ya wilaya ya Magu imetambuliwa kuwa ni mia moja na nane kati yao wanawake ni arobaini na saba na wanaume ni sitini na mmoja.

Amesema mbali na kuwatambua walemavu hao, pia halmashauri imeenda mbali zaidi kwa kuwapatia huduma za afya walemavu hao ikiwa ni pamoja na kuwapatia mafuta maalumu ya kulainisha ngozi na kuwapelekea mahali walipo kupitia ofisi ya ustawi wa jamii na uongozi wao.

Aidha ameongeza kuwa halmashauli hiyo pia imeanzisha kliniki ya watu wenye ulemavu wa ngozi katika hospitali ya wilaya ya Magu ambao wanafanyiwa uchunguzi katika ngozi zao ili kubaini dalili za awali za saratani ya ngozi na kuwapatia rufaa kwenda katika hospititali za rufaa ili kupata tiba mapema. EndS


Source: E

Ed:Im

Date February 16,2013

DODOMA

Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo  Pinda amesema   serikali itasaidia  kutekelea mpango wa maboresho  wa jeshi la polisi ili jeshi hilo liendelee kuwa kimbilio la raia wema.

Waziri mkuu pinda emetoa kauli hiyo wakati akifunga mkutano wa maafisa waandamizi wa jeshi la polisi nchini katika ukumbi wa msekwa  mjini Dodoma.

Aidha amesema kuwa jeshi la polisi linalohaja ya kuwashirikisha raia wakati wote, kuwapenda kwani raia wanaweza kuwa chanzo kikubwa cha kukabiliana na vitendo vya uhalifu badala ya kutengeneza mazingira yatayowafanya raia kuwa maadui wa polisi na hivyo inawezekana endapo jeshi la polisi likijenga misingi ya mabadiliko ya kifikra na kuwa na mtazamo mpya unaendana na wakati wa sasa.

Kwa upande wake waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dk Emmanuel Nchimbi amesema jukumu la ulinzi na usalama wa raia ni la kila mtu takita jamii huku akitoa wito kwa jamii kulisaidia jeshi hilo katika kukaribiana na vitendo vya uhalifu hapa.


 

Source: E

Ed:Im

Date February 16,2013

KIGOMA

Mwenyekiti  halmashuri  wilaya ya kasulu mkoani Kigoma  Bw Wiliam Nusuli amesisitiza umuhimu wa elimu kwa watoto huku akiwakumbusha wananchi kuendelea kuchangia mfuko wa maendeleo wa elimu wiyani kasulu.

Nusuli ametaja malengo ya uanzishaji  mfuko huo wa maendeleo ya elimu wilayani kasulu kuwa ni pamoja na kuwasaidia  kuwasomesha watoto wafamilia zisizokuwa na uwezo  ambao wameshindwa kuendelea na  masomo katika ngazi mbali mbali baada ya kuchaguliwa.

Naye afisa elimu Sekondari wialya ya Kasulu Patrick Athanas amewaagiza wakuu wote wa shule za sekondari wilaya ya kasulu na buhigwe kuwasilisha taarifa ofisini kwake kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao hawajaripoti hadi sasa shule wazizopangiwa ifikapo February 28 ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wazazi na walezi wa wanafunzi hao.


Source: E

Ed:Im

Date February 16,2013

SERENGETI

Watu wasiojulikana wakiwa na bunduki wilayani serengeti mkoani mara wamepora ng’ombe zaidi ya mia moja waliokuwa wakichungwa ndani ya hifadhi ya Serengeti.

Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Mara Japheti Lusingu amesema watu hao wakiwa na bunduki majira ya saa kumi na mbili jioni waliwatishia kuwauwa watu waliokuwa wakichunga ng’ombe hao endapo wangepiga kelele na ndipo walifanyikwa kuwapora ng’ombe hao na kutoweka nao pasipojulikana.

Lusinga amewataja watu walioporwa ng’ombe hao waliokuwa wakichunga kuwa ni pamoja na Suzana Juma mwenye umri wa miaka arobaini na mitatu na Nchama Peter wote wakiwa wakazi wa kijiji cha bolanga ambapo ng’ombe hao ni mali ya Juma Kasimu na peter Kasimu.

Jeshi la polisi linafanya juhudi za kuwatafuta ng’ombe hao kwa kushirikiana na wananchi ikiwa ni pamoja na kuwakamata watu waliohusika na uporaji huo.

 

 

                                      

HABARI ZA KIMATAIFA

 


 

Source: E

Ed:Im

Date February 16,2013

CAIRO

Naibu Mkuu wa chama cha Uhuru na Uadilifu tawi la kisiasa la harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri amesema kuwa wananchi wa Misri wana uwezo wa kulinda masanduku ya kura.

Usam al Ariyan Naibu Mkuu wa chama cha Uhuru na Uadilifu ameeleza kuwa matamshi ya baadhi ya shakhsia juu ya kuweko mahudhurio ya chini katika uchaguzi ujao yanaonyesha kutohisi majukumu watu hao.

 Amesema makundi yote yanapaswa kufanya juhudi za kukidhi matakwa ya wananchi na kwamba yule anayelinganisha hali ya mambo ya sasa ya Misri na ile ya kabla ya Januari 25 yuko katika ndoto.

Al Ariyan amesisitiza kuwa wananchi wa Misri wana uwezo wa kulinda kura zao mbele ya udanganyifu wa aina yoyote ile na kwamba hawatatoa mwanya wa kutokea jambo hilo.


Source: E

Ed:Im

Date February 16,2013

KIGALI

Rwanda inalenga kupata mapato ya dola za kimarekani milioni 317 kutoka kwa sekta ya utalii mwaka 2013.

Akieleza mpango huo kwenye mkutano na waandishi wa habari, mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Rwanda RDB Clare Akamanzi amesema nchi hiyo imeshuhudia ukuaji mkubwa wa setka ya utalii katika kipindi cha miaka sita iliyopita.

Ameongeza kuwa ukuaji huo umetokana na mazingira mazuri ya biashara ambayo yamesaidia kuimarisha soko na miundo mbinu ya utalii.

Sekta ya utalii ilichangia sehemu kubwa zaidi ya mapato ya fedha za kigeni ya Rwanda mwaka 2012 na kuongeza nafasi nyingi zaidi za ajira nchini humo. Mwaka 2012 nchi hiyo ilipata dola milioni 281.8 za kimarekani ikilinganishwa na mapato ya dola milioni 251.3 mwaka 2011.


 

 

Source: E

Ed:Im

Date February 16,2013

PRETORIA

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini na nyota wa Olimpiki,Oscar Pistorius, amefikishwa mahakamani akikabiliwa kwa madai ya kumuua mchumba wake baada ya kupigwa risasi akiwa nyumbani kwa Pistorius mjini Pretoria.

Pistorius aliangua kilio baada ya viongozi wa mashtaka kusema kuwa wataiambia mahakama kuwa mauaji ya mchumba wake yaliyotokea nyumbani kwake yalikuwa yamepangwa.

baada ya kufikishwa maghakamani , wakala wa Oscar alikanusha madai hayo vikali.

Ombi la dhamana ya mkimbiaji huyo limehairishwa hadi Jumanne wiki ijayo,na yuko mbaroni kwa sasa.

Mwaka jana Pistorius alikuwa mwanariadha wa kwanza mlemavu kuruhusiwa kushindana na wanariadha wengine wasio na ulemavu kwenye micheco ya Olimpiki, kwam kutumia miguu bandia.

 

 

 


 

Source: E

Ed:Im

Date February 16,2013

HAVANA

Serikali ya Venezuela imechapisha picha za mwanzo za rais wa taifa hilo Hugo Chaves anaekabiliwa na ugonjwa wa saratani tangu afanyiwe upasuaji mjini Havana, nchini Cuba miezi miwili iliyopita.

Picha hizo zilizotolewa zinaonamuonesha kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 58 akitabasamu lakini sura yake ikiwa kama imevimba.

 

 Alikuwa amelala katika kitanda cha hosiptali huku mabinti wake wawili wakiwa pembeni na mwenyewe akisoma gazeti la serikali ya Cuba Granma.

 

Habari zinaesema kuwa rais huyo anakuwa katika wakati mgumu katika kuzungumza lakini anaweza kuelewa mambo yanayoendelea


 

No comments: