Wednesday, November 21, 2012

RUSHWA INAZITAFUNA HALMASHAURI NCHINI TANZANIA


Baada ya kubaini na hatimae kukiri kuwa idara za serikali za mitaa zinanuka kwa rushwa nchini Tanzania Taasisi ya kuzuia na kupambana na rusha nchini TAKUKURU imeanza kutoa mafunzo kwa kamati za maadilii za halmashauri za wilaya, manispaa, miji na majiji nchini

Mkoani Kigoma mafunzo hayo yameanza jana yakihusisha kamati za maadili kutoka miko aya Kigoma, Kagera na Shinyanga ambapo zaidi ya washiriki 30 wamehudhuria mafunzo maalumu ya mkakati wa pili wa kupambana na Rushwa NASCAP II

Jumla ya halmashauri kumi na moja (11) zimetuma wawakilishi kushiriki mafunzo hayo

Cha kujiuliza ni je, kamati hizi za maadili zina nguvu gani ya kisheria ya kudhibiti vitendo vya rushwa miongoni mwa watumishi wa serikali za mitaa ambao wanatajwa kujilimbikizia mali kuliko hata kiwango vha mishahara yao na umri katika utumishi?

Je ni nani mteuzi wa kamati hizi ambazo miongoni mwa wajumbe wake nao ni watuhumiwa wa vitendo vya uvunjifu wa maadili, uzembe kazini na Rushwa?

Je! Kanuni ya uhakiki wa mali za watumishi ambayo imekuwa ikiwaandama wabunge na mawaziri, huku chini inatumika kudhibiti utajiri wa ghafla mara tu mtu anapopata ajira au uwakilishi wa wananchi katika halmashauri za wilaya, miji, manspaa na Jiji?

Hebu tuchangie hoja hii,

“kwa kuwapa mafunzo wajumbe wakamati za maadili za halmashauri, TAKUKURU itafanikiwa kudhibiti Ruswa katika ofisi za utoaji wa huduma kwa wananchi hususani idara ya Mipango, Utumishi, Ugavi, fedha na Afya? “

Tuma maoni yako kupitia srfm2011@gmail.com au tuma maoni yako kwenye kisanduku cha maoni chini ya habari hii, pia unaweza kupiga simu namba 0786200518 au 0763837396

UNAO UHURU WA KUSEMA CHOCHOTE NASI TUTAPEPERUSHA MAONI YAKO KWA UMAKINI

STANDARD RADIO FM

SAUTI YA WASIO SIKIKA

 

1 comment:

Anonymous said...

Mie naona hiyo siyo dawa, Rushwa ni moyo wa mtu, kwani hao wajumbe wao ni salama? sina hakika