Tuesday, November 20, 2012

KESI YA MWIGULU DHIDI YA CHADEMA YAPIGWA TAREHE


Halima jamal
Singida

KESI inayowakabili viongozi wawili wa CHADEMA taifa dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Iramba magharibi na Naibu Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mwigulu Chemba, imeaahirishwa hadi Desemba 17 mwaka huu, kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na mwanasheria wa serikali kuugua.

Imeelezwa mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi, Ruth Massamu, kuwa mwanasheria huyo wa serikali Maria Mdulugu anayesimamia kesi hiyo ni mgonjwa.

Viongozi hao ambao wanatuhumiwa kutumia lugha ya matusi katika mkutano wao ni Waitara Mwikwabe (37) afisa sera na utafiti makao makuu paoja na Dk.Kitila Mkumbo mhadhiri wa chuo kikuu Dar-es-salaam na mshauri wa CHADEMA.

Kutokana na hali hiyo, mahakama hiyo pamoja na wakili wa washitakiwa Raymond Kimu,walikubaliana kesi hiyo ianze kusikizwa.

Kwa mujiubu wa mwanasheria wa serikali, Seif Ahmed,alidai kuwa washitakiwa bila halali, walimtusi mbunge Mwigullu kuwa ni malaya, mzinzi na mpumbavu huku akijuwa wazi kuwa kitendo hicho ni kinyume na sheria.

Seif alidai kuwa washitakiwa walitenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nguvumali kwa lengo la viongozi wa CHADEMA kuzungumza na wananchi.

No comments: