Saturday, November 17, 2012

HATARI YA MCHEZO WA POOLL

   

   Na Phesthow Sanga.

   Iramba  

Watoto  hawa  hawasomi?

Siku hizi si ajabu wala aibu kuwakuta watu wazima katika michezo mbalimbali muda wa kazi, na michezo inayovuma kwa sasa ni pamoja na mchezo wa POOL ambao nchi nyingine huchezwa na matajiri tena wakati wa mapumziko ya jioni

Kwa Tanzania hili ni kinyume chake kabisa, pool huchezwa na vijana pamoja na watoto tena hohe hahe, wale wasio na ajira, wale ambao ama wana migogoro ya kifamilia na wenye tabia mbaya katika jamii yao hususani ulevi wa viloba, gongo nk

Nikiwa katika mji wa Kiomboi huku ikipita huku na huku  nakutana  na watoto wa kiume wanatembea wawili watatu wengine wana  karanga vikapuni wanauza.

Katika  hali ambayo sikuwa  na jibu nilipata jibu haraka  nilipofika  katika  eneo la stendi  kuu ya mabasi kiomboi  ambapo kuna sehemu kumewekwa meza za Pool na watu hucheza mchezo huo tena  mbaya zaid hucheza kamari  ambapo husababisha  mara  nyingine Ugomvi kutokea.

 “Tafadhali wazazi na wote  tunao husika  na malezi  ya watoto, Tushirikiane tulivunje jinamizi hili kwa watoto ili tuondoe wimbi la watoto kuwaita  ni watoto wanaoishi katika  mazingira  hatarishi.” Pooll ni mchezo mzuri hata hivyo haufai kwa watoto tena wanafunzi

                                                 Mwisho.

No comments: