Wednesday, November 7, 2012

ASKOFU BALINA AAGA DUNIA



Na Edilitruda Chami

Askofu wa kanisa katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu Aloysious Balina amefariki dunia jana majira ya saa 5 asubuhi katika hospitali ya Bugando mkoani Mwanza alikokuwa akitibiwa kwa muda mrefu.

Marehemu  Askofu Balina alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa muda mrefu hadi mauti yalipomkuta.  Alizaliwa Julai 21, mwaka 1945 na amefariki akiwa anamtumikia Mungu Kwa miaka 45 ya upandre na miaka 27 ya uaskofu.

Mwili wa marehemu utazikwa katika kanisa la mama Maria mfanyakazi - Ngokolo mkoani Shinyanga siku ya jumamosi saa nne asubuhi.{MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMINA}

No comments: