Wednesday, November 28, 2012

CHANGAMOTO KATIKA IDARA ZA AFYA-UWAJIBIKAJI DUNI


NA  Phesthow   sanga 
Shirika   lisilo  la kiserikali   {SIKIKA] ambalo  ofisi   yake  kuu  ipo  Dodoma   na  ambalo  linajihusisha  na mambo  ya   wizara  ya  Afya  nchini   hivi  majuzi   limemaliza   kazi  zake   za  Ufuatiliaji  wa  Uwajibikaji   jamii, katika  Uwajibikaji   wa  Watoa  huduma   na  wenye  Mamlaka  katika  kuhakikisha   haki  za  Binadamu   na   jamii   Zinapatikana .

 Timu  hiyo  ambayo  iliundwa  na wajumbe  waliochaguliwa  katika  makundi   mbali mbali  ya  jamii,wakiwepo  pia madiwani  wa  kamati  ya  Huduma  za  jamii  pamoja  na  Viongozi  wa  Dini  na  Madhehebu   yaliyopo   katika   wiliaya  ya  Iramba  walianza   kazi  tangu  Okt 25 na kumaliza nov 24  mwaka  huu.

Akiongea  na  Wanahabari,   Mkuu   wa  Ofisi  ya  Sikika  Dodoma   bw. Patrick N.Kinemo ,Amesema  kuwa  shirika   hilo katika   miaka yake   kumi  tangu  lianzishwe  limejikita  Na  mambo  ya  Wizara  ya  Afya  ikwemo  kufuatilia  mambo  ya  madawa, Raslimali Watu ,vifaa  Na  Mambo  yote  yanayohusu  wizara  ya  Afya  kwa  Ujumla  .

Akizitaja   kero  na  mapungufu  pamoja  na  mambo  mengine  yaliyoibuliwa   wakati  timu ya {PSAM} Ilipokuwa  ikitembelea  zahanati   Na  Vituo  vya  Afya   katika  wilaya  ya Iramba   Ni Pamoja  na  Akina mama  Wajawazito   kutozwa  gharama  za  Kadi   za  klinik  iwapo  mama  huyo  atakuwa  amepoteza  kadi  yake .

Hali hiyo ilkutwa  katika  Kituo  cha  Afya  cha  Mgongo  ambapo  Wananchi  walitoa  malalalmiko  yao  kuwa  wanalipizwa  tshs. Elfu Tano  kwa  mjamzito  kama  kapoteza  kadi  yake , pia  malalamiko kama  hayo  yalitolewa  na   wananchi  katika  Zahanati  ya  Shelui  kuwa   wajawazito   hulipizwa shilingi   Elfu  mbili  kama  amepoteza  kadi yake  huku  katika  kituo  cha  Afya  cha  Ndago  Akina mama hulipizwa  tshs Elfu moja  kwa  upotevu  wa  kadi.

 Mambo   Mengine  ni  Upungufu  mkubwa   wa  Watumishi , Uchakavu  wa  Majengo , magari  katika  Vituo  vya  Afya , Madawa , Vifaa Tiba,  Ulinzi , Usimamizi  wa Fedha ,matibabu ya  Wazee  mizani  za watoto katika  Zahanati nyingi , Semina  kwa  watoa  Huduma.

Aidha   Timu ya public  service  accountability  monitoring {PSAM}  Imegundua  madawa  ya thamani  ya tshs .1,342,400.yameharibika  na kutofaa  tena  katika  matumizi  ya  Binadamu  bado  Hayaja  teketezwa  na kuchomwa   kama  ilivyoagizwa  na  amri {order}  no.244  ya mwaka 1997  na  hakuna  hatua   zozote Zilizochukuilwa   na  Uongozi wa  Halmashauri  hiyo.

Kutokana  na  taarifa  ya  Timu  ya  PSAM,  Iligundua  pia  Akiba  kubwa  ya  Vyandarua  katika  stoo  ya hospitali   ya  wilaya  Neti  ambazo  hazijagawiwa ;4811 ambazo  zilitolewa  na MEDA , Tangu  Januari 2011; na  uongozi  wa Halmashauri  upo  na  hakuna  hatua  yoyote  ilyochukuliwa  kuhusiana  na vyandarua  hivyo .

Akijibu  na kutolea  Ufafanuzi   kuhusu  Taarifa  Iliyotolewa   na Timu  ya  psam   Kaimu  Mganga  Mkuu  wa  Wilaya  Dr.  Mbulu  alieleza  kuwa  katika  mambo yote  yaliyosemwa   yanatekelezwa  kulingana  na  bajeti ,aidha  alikiri  kuwa  mambo  Mengine Watayafuatilia ,kama  Utozwaji  wa  kadi  za  klinik  kwa  akina  Mama wajawazito

No comments: