Saturday, November 3, 2012

KIKWETE KUZURU MKOA WA SINGIDA


 
 
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta  Jakaya Mrisho Kikwete atafanya ziara ya siku mbili mkoani Singida kuanzia tarehe 4 hadi 5 Novemba mwaka huu wa 2012

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa Singida Dokta Parseko V.Kone wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake akifafanuzi  uwepo wa ziara ya Raisi mkoa wa Singida

Dokta Kone amefafanua kuwa Rais atatembelea Miradi mbalimbali ya barabara  pamoja na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa maji Singida mjini unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania pamoja na mkopo nafuu kutoka kwa wahisani

Hii ni mara ya kwanza kwa rais Kikwete kufanya ziara mkoani Singida tangu kumalizikia kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 uliomweka madarakani kwa kipindi cha pili na cha mwisho kwa mujibu wa katiba ya Tanzania

Hadi sasa Rais Kikwete yuko mkoani Manyara kwa ziara ya kikazi baada ya kutoka mkoani arusha ambako amefanya mikutano na viongozi na wananchi wa mikoa hiyo.

 

No comments: