Saturday, November 17, 2012

MAALIM SEIF ZIARANI KIGOMA


Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar na katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif  Sharif Hamad leo anaanza ziara mkoani Kigoma akifuatana na mwenyekiti wake wa taifa Ibrahim Haruna Lipumba

Akiwa mkoani Kigoma atafanya mikutano kadhaa ya hadhara ambapo leo atakuwa mjini Kasulu kuhutubia wananchi katika uwanja wa maengesho ya magari mjini hapa.

Uwanja huo unatumiwa na makamu huyo wa rais siku chache baada ya kamati ya ulinzi na usalama wilayani Kasulu kupiga marufuku matumizi ya eneo hilo lililopo katikati ya soko kuu kwa shughuli za mikutano ya kisiasa kwa hofu za kiusalama

Hadi sasa viongozi wa wilaya ya Kasulu na mkoa wa Kigoma wa Chama cha Wananchi CUF hawajasema maudhui ya ujio wa viongozi wao wa kitaifa mkoani Kigoma

Hata hivyo tetesi zinadai kuwa ziara hiyo ni sehemu ya kuvunja nguvu za Chama cha Demokrasia na Maendeleo pamoja an NCCR mageuzi mkoani humo

Mkoa wa Kigoma kwa sehemu kubwa wabunge wake wanatokana na vyama vya upinzani ambapo NCCR ina wabunge wane (4) Chadema mmoja (1) na CCM wabunge watatu (3)

Ziara hiy ya Maalim Seif na Lipumba inakuja pia siku chache baada ya Baba wa Upinzani mkoani Kigoma Dr. Aman Kaburu aliyekuwa kiongozi wa juu wa CHADEMA nchini aliyehamia CCM na kuwa mbunge wa Afrika mashariki, kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kigoma

No comments: