Friday, November 2, 2012

NITUNZE NIKUTUNZE


Edilitruda Chami Na Eufrasia Mathias

Singida ni mkoa uliopo katikati ya Tanzania na ni mkoa ambao una shida ya maji kwa sababu ya ukame kiasi kwamba baadhi ya maeneo hawalimi mazao yanayohitaji unyevunyevu na maji kwa muda mrefu kama mahindi, maharage na mbogamboga

Imani ya watu wengi Singida ni kwamba ni vigumu kuwa na ukijani katika mkoa huo kutokana na upungufu wa maji na mvua ambazo hunyesha kwa misimu isiyokuwa na mpangilio na wakati mwingine mvua kutokunyesha kwa muda mrefu

Ninachotaka kukuambia msomaji wa hiki ninachokiandika ni kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na ukijani katika mkoa wa Singida hasa kwa wale wajanja wanaojua matumizi ya rasilimali chache na adimu kama maji katika mkoa wa Singida

Sizungumzi kwa maneno tu ila kwa kile nilichokiona na kukishuhudia tena katikati ya mkoa wa Singida ambapo bustani ya mboga mboga imeng’aa na ukijani kama uliopo mwambao wa  bahari nzuri ndipo nikaamini kuwa kama wewe unashindwa kuwa na bustani kutokana na ukame kuna mwingine ana bustani naye anakuuzia mbogamboga unazokula kwako

“jaribu nawe uone!”

No comments: