Na Evarista Lucas
Singida
Mkuu wa wilaya ya Iramba Bwana Yahya Nawanda; amewaasa viongozi na wanachama wa
Klabu ya waandishi wa habari Singida(SINGPRESS
kuyafuata yale waliyoafikiana katika mkutano na kuhakikisha kuwa
hawaendi kinyume na mabadiliko hayo.
Akihutubia wanachama hao katika mkutano
wao wa marekebisho ya katiba ya SINGPRESS uliofanika katika kijiji cha Kiomboi
wilaya ya Iramba mkoani Singida; Nawanda aliwawataka wanachama hao kuwa mfano
mzuri wa kuigwa kwa kufuata maadili ya kazi yao .
“Siku hizi tasnia ya uandishi wa
habari imekuwa inaingiliwa sana
na watu na watu wasiokuwa na maadili
ambao ndio wanaofanya kazi hii na heshima mbele ya jamii, kwani uandishi
ni maadili.” Alisisitiza Nawanda.
Kwa upande mwingine Nawanda
aliwataka wanachama hao kuepukana na ushabiki wa kisiasa ili waweze kufanya
kazi yao kwa ufanisi zaidi na kwa kuzingatia
maadili ya kazi yao . “Baadhi yenu mmekuwa wanasiasa tena wa wazi
wazi. Mnafanya kazi ya viongozi wa
siasa. Mimi nawaasa mfuate maadili ya uandishi wa habari na kuachana na siasa.”
Nawanda.
Licha ya hayo
Nawanda aliwaomba wanachama hao kuandika pia mambo mazuri ambayo
yamefanyika hapa mkoani ikiwemo ujenzi wa hospitali ya kisasa ya rufaa,
barabara za lami na makazi bora.
“Tutawapa ushirikiano mkubwa
waandishi wa habari kwani nyie ni watu muhimu kuhabarisha Watanzania kile
tunachokifanya katika maendeleo ya mkoa wetu. Wasaidieni kuandika makundi
maalumu kama
vile walemavu, changamoto zao na ustawi wao kwa ujumla na sio kujikita
kwenye siasa tu. Sasa Tanzania
tunajua mwandishi bora ni yule anayejikita kwenye siasa tu.” Nawanda
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
SINGPRESS Bwana Seif Takaza alimshukuru mkuu huyo wa wilaya kwa kuitikia wito wa kuwa mgeni wa heshima
katika mkutano wao na pia kwa kuwapatia ukumbi uliowawezesha kuikamilisha kazi
hiyo muhimu kwa maendeleo ya Klabu.
“Hii ni awamu ya pili kwa waandishi wa habari
kufika katika wilaya ya Iramba awmu ya
kwanza ilikuwa ni Mei 3 mwaka huu siku ya uhuru wa vyuombo vya habari ambapo
tulikwenda kwa Wahadzabe na kutoa msaada wa chakula na vifaa vya shule. Leo
tena awamu ya pili tunafanya mkutano huu hapa.
Katika mkutano huo uliojumuisha wanachama kumi
na saba (17) wa SINGPRESS wanachama walipata fursa ya kuipitia kwa umakini
katiba hiyo na baadhi ya vipengele vilivyoongezeka katika katiba hiyo.”
No comments:
Post a Comment