Sunday, August 5, 2012

MATUKIO KATIKA PICHA

MELI ILIYOUWA MAELFU YA ABIRIA KATIKA BAHARI YA HINDI HIVI KARIBUNI, AJALI HII HUENDA IMEKUWA SOMO AU FUNZO KWA WATANZANIA AMBAO LICHA YA KUSHUHUDIA KUTOKUWEPO KWA NAFASI KATIKA VYOMBO VYA USAFIRI HUSUSANI TRENI, BASI NA MELI TUMEKUWA NA TABIA KING'ANG'ANIZI KUPANDA TU HUKU TUKIFURIKA MAWAZO NA TAMAA YA SHIDA ZETU TU, NA PINDI IKITOKEA AJALI LAWAMA ZOTE KWA SERIKALI AU DREVA AU BAHARIA, JE HII NI SAWA

Binadamu ni kiumbe wa ajabu hebu tembelea barabara kuu ya Kigoma-Mwanza na Kigoma -Dar utashangaa baadhi ya mabasi yakibeba abiria lukuki (kuzidi kiwango) abaria kulazimishwa kusimama au kuwekewa vigoda na hata benchi katika korido la basi, lengo ni kujaza abiria wengi kuzidi kiwango kilichopangwa au uwezo wa gari husika, Je hii ni Sawa
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++=========\
======================================================================
MAHASIMU WAWILI WALIOKUWA MARAFIKI WAKATI WA VITA VYA KUIPAMBANIA UGANDA, SI WENGINE NI DR. BESIGE NA MSEVENI


Mvumilivu hula Mbivu, Wahenga walisema, Besigye ni miongoni mwa wanasiasa wavumilivu, lengo ni kuwa rais wa Uganda, je Anapigania haki za weaganda au manufaa ya familia na uko wake? Je Mseveni naye alipokuwa msituni huko Kagera maeneo ya Bunazi na kwingineko porini ndani na nje ya Uganda alikuwa na nia thabiti ya kuwasaidia waganda? kama ndiyo kwanini leo haoni kuwa ametimiza wajibu wake na hapo alipofikia awaachie na wengine? TAFAKARI
====================================================================
====================================================================
MSANII ANAYETEKA ANGA LA MZIKI WA TANZANIA, INAELEZWA KUWA DIAMOND KWA SASA ANAPENDWA NA MASHABIKI WA MUZIKI KULIKO MSANII MWINGINE YEYOTE KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2012


Wasanii wa tanzania wanaendelea kushika kasi, ukisafiri kwenda nchi za DRC, Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya na Sudan kusini hutashangaa kusikia nyimbo za wasanii wa tanzania zikiimbwa katika vyombo vya habari radio na Runinga, je wasanii wetu wanalijua hilo, na je soko hilo la muziki katika nchi za maziwa makuu lina tija kwao?
==================================================================

Msanii Elizabeth Michael (LULU) anayesota Rumande kwa tuhuma za kumuunga msanii mwenzake KANUMBA anayetajwa kuwa licha ya umri wake kuwa mdogo, maumbile yake yalimponza na kujikuta akimega tunda na wasanii mbalimbali akiwemo Kanumba mwenyewe. Inadaiwa kifo cha Kanumba kilitokana na ugomvi wa kimapenzi na LULU, Wasanii wadogo wa kike huenda inawauma kumuona mwenzenu akisota kwa tuhuma za mauaji, lakini tunaamini kuwa mnaumia sana zaidi kutokana na tuhuma kuwa wasichana wadogo wanaojiunga na fani hii ya sanaa mmekuwa mkitumiwa na wasanii wakubwa na mastaaaaa kama viburudisho, Huu ni mwanya adhimu wa kila msanii msichana kujitafakari

No comments: