Thursday, August 9, 2012

TANZANIA KUPATA MAFUTA ZIWA TANGANYIKA

Mbunge wa Kigoma Kusini kwa tiketi ya NCCR David Kafurila, Jimbo lake ni miongonim wa maeneo yenye madini, Chumvi Uvinza na utafiti wa mafuta katika mto Maragalasi eneo la Nguruka
==============================
Changamoto ya uwekezaji katika sekta ya madini , ukosefu wa masoko na uzalishaji duni wa bidhaa za madini yanayozalishwa na wachimbaji wadogo wadogo nchini Tanzania inatajwa kuwa chanzo cha umasikini nchini humo
Hayo yamebainishwa na naibu waziri wa Nishati na madini nchini Tanzania Bw. Steven masele wakati wa ziara yake mkoani Kigoma kukagua utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa umeme katika wilaya za Kasulu na Kibondo pamoja na utafiti wa madini mkoani humo
Bw. Masele amebainisha kuwa serikali pamoja na utungaji wa sera inao wajibu sasa wa kuwatafutia masoko wachimbaji wadogowadogo wa madini hususani yale ambayo ni malighafi kwa uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za viwandani
‘Sisi kama serikali tunawajibika kuwawezesha kupata masoko ili msaidie kukuza pato la taifa letu, madinikama chokaa kwa sasa yanahitajika sana kwa ajili ya kuhuisha madini mengine, mfano NIKEL kule Kabanga Ngara mkoani Kagera na kule Bariadi mkoani SIMIWI, hata Saruji pia inahitaji chokaa, kwahiyo mkijua masoko yaliko mtapiga hatua’ alisisitiza Masele
Aidha Naibu Waziri huyo wa Nishati na madini amebainisha  kuwa Tanzania kwa kushirikiana na makampuni mbalimbali ya Kigeni inaendesha utafiti wa mafuta katika ziwa Tanganyika na mto Maragalasi magharibi mwa Tanzania
“tunnatarajia kuwa endapo mafuta katika ziwa Tanganyika na mto maragarasi yatapatikana, wenyeji wa maeneo hayo wawe wa kanza kunufaika, Tanzania haina sabau ya kuendelea kuwa masikini wakati kuna madini, na endapo mafuta yakipatikana basi tumeukata, kwani hakuna nchi yenye mafuta duniani ikaendelea kuwa masikini, alisisitiza Masele akiongea na wananchi wa mji wa Kasulu.
Endapo mafuta yatapatikana nchini Tanzania, afrika mashairiki itakuwa miongoni mwa mataifa tajiri barani afrika endapo sera na uendeshaji wa migodi utazingatia mahitaji ya wananchi wake
Hata hivyo imeelezwa kuwa  uwezo mdogo wa kitaaluma wa watanzania katika sekta ya madini, tatizo la urasimu katika upatikanaji wa leseni kwa wachimbaji wadogowadogo pamoja na mikataba isiyo na tija inayotolewa kwa wachimbaji wakubwa wa madini ni kikwazo kwa uchumi wa Tanzania
“Wizara yetu, tumeamua kupitia upya mikataba yote ya madini ili kuhakikisha Tanzania inanufaika na maliasili hiyo, tutahakikisha pato la taifa linalotokana na madini linaongezeka na mwekezaji ambaye hataki aondoke mwenyewe” Naibu waziri alisisitiza
Kwa Upande wake wabunge wa majimbo ya Kasulu mjini Moses Machali na David Kafurila wa Kigoma kusini wameeleza kuwa na imani na serikali ya Rais Jakaya Kikwete NA KUBAINISHA KUWA KINACHOITATIZA SERIKALI NI KUSHINDWA KUWACHUKULIA HATUA MAFISADI
Aidha uchimbaji wa madini nchini Tanzania umekuwa ukigharimu uharibifu mkubwa wa mazingira hali inayotajwa kuwa hatari kwa ustawi wa binadamu na viumbe vingine nchini humo.



No comments: