Na, Doris Meghji
Singida
Mgomo wa walimu nchini kutoathiri zoezi la sensa ya watu na makazi mkoani Singida linalotarijiwa kufanyika Agosti 26 mwaka huu imefahamika.
Akiongea ofisini kwake mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi mkoa wa Singida Bwana Nestory Mazinza alisema licha ya mgomo wa walimu uliodumu kwa muda wa siku tatu hatoataathiri zoezi la sensa ya watu na makazi mkoani Singida huku maandalizi ya zoezi hilo kuendelea vizuri ambapo jumla ya makalani elfu nne(4000) wanatarajiwa kupewa mafuzo Agosti Tisa mwaka huu
“uvumi wa walimu kugoma mkoa wa singida alijaathiri chochote kwa sababu kila tunajaribu kufanya upembumbuzi inasemekana kwamba walimu watashiriki vizuri tu katika zoezi la sensa.” Alisisitiza Mazinza
picha
kulia aliyeshika kipeperushi cha Sensa ni Mratibu wa Sensa wilaya ya Manyoni Edga Madeje,kushoto ni mjumbe wa kamatiya sensa manyoni Nelson Mapunda wakimsiliza mwenyekiti wa kamati ya sensa mkoa wa singida.akitoa elimu hiyo tarafa ya Chikuyu wilayani Manyoni (picha na Doris meghji)
Aidha kwa upende wa maandalizi ya Zoezi hilo amesema suala la upembuzi wa makalani wa sensa ni zaidi ya asilimia tisini ya zoezi hilo limekamilika hivyo wanasubiri tu kamati za sensa kupitia na kutoa baraka kwa majina ya watu watakao kuwa makalani wa sensa ili kupatiwa mafunzo agosti tisa mwaka huu.
wanafunzi tarafa ya Itigi wilaya ya manyoni wakisikiliza ujumbe wa sensa katika uzinduzi wa elimu ya sensa wilayani manyoni Julai 26 iliyofanywa na mwenyekiti wa kamati ya sensa mkoa wa singida DR. Parseko Kone ambaye ni mkuu wa mkoa wa singida.
Naye mratibu wa sensa ya watu na makazi wilaya ya Manyoni Bwana Edga Madeje amesema wilaya yake inatarajiwa kutoa mafunzo kwa makalani mia nane arobaini na nane(848) kati ya hao sitini na sita (66) ni wasimamizi wa sensa na makalani mia nne sitini (460) wa dodoso refu na mia tatu ishirini na tatu makalani wa dodoso fupi
Wilaya ya Manyoni ina jumla ya kata thelathini(30) katika kila kata wanaratijia kupeleka wasimamizi watano ili kufanika zoezi hilo la sensa ya watu na makazi amesistiza mratibu Madeje kwa maandalizi ya zoezi hilo wilayani humo.
Hata hivyo Mratibu wa sensa mkoa wa Singida Bwana Nestory Mazinza ametoa wito kwa walimu mkoa wa Singida kushiriki vyema katika zoezi la sensa kutoleta mgono, kwani wakileta mgono watauangusha mkoa wa singida ikiwa takwimu za sensa ni kwa maendeleo ya mkoa na Taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment