“Nimeteseka sana, nimetengwa sana, na
nimeumizwa sana pamoja na kuwaumiza wenzangu, yote haya ni kwa sababu ya
matumizi ya madawa ya kulevya, pombe kali hasa viloba hadi akili yangu
ikaharibika nikajikuta nimekuwa mwehu nikitembea hovyo mitaani, kutukana na
hata kupigana, hakika kwa sasa ninalo funzo kwa vijana wenzangu”
Hii ni Kauli
ya kijana mmoja kutoka Dar es salaam ambaye sasa anatibiwa na kutunzwa katika
kijiji cha Marumba wilayani Kasulu ambako alifikishwa na ndugu zake miezi
kadhaa iliyopita baada ya kuugua ugonjwa wa akili na sasa akili yake japo kwa
mwendo wa kinyonga inaanza kurejea.
Matumizi ya
pombe kali VILOBA ni moja ya chanzo cha vijana wengi kuwa na matatizo ya akili
na hata kupoteza afya ya mwili pia, si ajabu kuwakuta wapenzi na wanywaji wa
viloba wakiwa maumbile yaliyokonda na kuchoka, kuungua midomo na hata kunyonyoa
nywele, kukosa uwezo wa kufikiri na mwili kukosa nguvu
Si ajabu
kumkuta kijana mpiga viloba akitetemeka mwili kila wakati anaposhika au kubeba
chochote mikononi mwake, wengu wanashindwa hata kufanya kazi yoyote
Taifa limepoteza
nguvu kazi kutokana na viloba na ulevi mwingine wa kupindukia pamoja na
matumizi ya madawa ya kulevya,
Hii ndiyo sababu shirika la kitawa la BROTHERS OF CHARITY
liliamua kuanzisha kitengo cha afya ya akili na kuanza kutoa tiba ya magonjwa
hayo pamoja na matunzo ya kijamii na kisaikolojia kwa wagonjwa wa akili maarufu
kama WEHU.
PICHA
No comments:
Post a Comment