Wednesday, August 15, 2012

WAKIMBIZI WA BURUNDI WASUSA KURUDI KWAO

Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Burundi walioko katika kambi ya wakimbizi ya Mtabila mkoani Kigoma wakisikiliza hotuba za kuwahamasisha kurejea nchini kwao

Hadi sasa zoezi la kuandikisha wanaohitaji kurejea kwa hiyari linaendelea ingawa mwitikio ni mdogo sana na baadhi ya wakimbizi wamekuwa wakitoa kauli kuwa hawako tayari kurudi
Burundi

Picha na. Prosper Kwigize

Na. Omary Mbwambo,
Kigoma


Wahenga walisema mkataa kwao ni mtumwa napia wakasema jasiri haachi asili

Misemo hii inaweza kukubalika katika mazingira Fulani napia inaweza kutokubalika katika sehemu zingine kulingana na mazingira na tabia za watu Fulani ama historia ya mahali husika

Tumeshuhudia serikali ya Tanzania kupitia kwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi na mwenye mamlaka  na dhamana ya wakimbizi hapa  chini Tanzania hapo Agost 1 mwaka huu amewafutia hadhi wakimbizi wapatao 38050 waishio katika kambi ya wakimbizi ya mtabila iliyopo wilayani kasulu mkoani Kigoma ikiwa ni hatua za mwazo za kuruhusu kufungwa kwa kambi hiyon ifikapo Disemba 31 mwaka huu.

Uamuzi wa kuifunga kambi hiyo umekuja baada ya mashirika mbalimbali ya kimataifa duniani  pamoja na nchi ya Burundi kuudhihirishia ulimwengu  kuwa kilicho wafanya wakimbizi hao kukimbilia nchini Tanzania sasa hakipon tena nchini Burundi kwa maana ya kuwa sasa amani nchini Burundi imekwisha rejea na hakuna vita vya ukabila ama vita vya aina vyotyote katika hiyo.

Baada ya zoezi hilo la kufutia hadhi wa kimbizi hao waishio katika kambi hiyo ya mtabila  sasa zoezi linaloendelea ndani ya kambi hiyo ni wakimbizi hao kurejea nchini kwao kwa hiari  ili kuruhusu kufungwa kwa kambi hiyo napia kutoa nafasi kwa wakimbizi hao kwenda nchini kwao kwa dhumuni la kufanya kazi katika nchi yao kwa dhumuni la kuijenga nchi yao  badala ya kuendelea kuishi ukimbizini katika nchi ya Tanzania.

Nchi ya Burundi ,Tanzania sambamba na Shirika la kuhudumia wakimbizi duniani  la UNHCR wamekubaliana kuhakikisha wakimbizi hao wanarejea nchini kwao katika hali ya usala na kiutu zaidi huku wakipewa misaada mbali mbali kutoka kwa mashirika yanayowahudumia ili kutoa nafasi ya kufungwa kwa kambi hiyo kama makubaliano yaliyofanyika baina ya Burundi,Tanzania  na shirika la kuhudumia wakimbizi.

Kutokana na mazoezi hayo kufanyika ndani ya kambi hiyo wakimbizi hao wametakiwa kwenda kujiandikisha katika vituo ndani ya kambi hiyo nakuwa tayari kwa kurejea nchini kwao kwa hiari badala ya kuendelea kukaandani ya kambi hiyo huku kukiwa hakuna huduma mbalimbali kama kufungwa kwa shule ndani ya kambi hiyo

Wakimbizi hao wametakiwa kushirika katika zoezi hilo badala ya kuonesha kukaidi zoezi hilo la kujiandikisha nakuwa tayari kurejea nchini kwao ama kufikiria kuwa serkali ya Tanzania itabadili msimamo wake juu ya kuifunga kambi ya Mtabila

Kwaupande wao wakimbizi waishio katika kambi hiyo baadhi yao wameonesha kutii kauli hiyo ya kujiandikisha na kuwa tayari kurejea nchini kwao tayari kwa kulijenga taifa la Burundi kwa kuammini ya kuwa nchi yao ya Burundi itajengwa na warundi wao wenyewe

Pia kuna baadhi ya wakimbizi ndani ya kambi hiyo wao wameonesha kutokuwa tayari kurejea nchini kwao kwa kueleza kuwa kutokana na taabu walizo zipata ama kutokana ma historia za kule walipotoka  napia kutokana na habari mbalimbali katika vyombo vya habari pamoja na watub wengine waliokwisha kurejea nchini kwao zinasema nchini Burundi bado kuna machafuko ya chini chini

Wapo wengine wanaosema kuwa suala hili la wao kurejea nchini Burundi limekuja kisiasa zaidi na halija waangalia wao ambao wengi wao wamepoteza ndugu na jamaa  na marafiki katika vurugu hizo zinazoendeklea nchini Burundi

Baada ya majibu hayo kutoka kwa kwa wakimbizi hao niliwataka japo waniambie kama wapotayari kurejea nchini kwao napia wanalichukuliaje suala zima la wao kurejea nchini kwao kwa hiari katika kipindi hiki kilichobaki kabla serikali ya Tanzania na mashirika ya kimataifa hayajawachukulia hatua za juu zaidi, wakimbizi hao walijibu kuwa wao kwa namna yoyote ile hawapo tayari kurejea nchini kwao kwasasa kulingana na mateso waliyoyapata muda ule na haya yanayoendelea nchini kwao

No comments: