Wednesday, August 8, 2012

TANESCO KIGOMA YAPEWA SIKU 30 KUWAPA UMEME WATEJA

Mhe. Steven Masele akiwa katika sura ya hasira baada ya kushuhudia makosa na uzambe wa kiufundi katika mradi wa usambazaji wa umeme wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Ni baada ya kushuhudia ujenzi hafifu wa mtandao wa usambazaji wa umeme katika baadhi ya mitaa na kuelezwa na wabunge pamoja na viongozi wa CCM kuwa kuna urasimu mkubwa wa usambazaji wa umeme kwa wananchi

Naibu waziri wa Nishati na madini, Mhe. Masele akiongea jambo na viongozi wa wilaya ya Kasulu baada ya kukiri kukerwa na uongozi wa TANESCO Kigoma kabla ya kutoa amri ya siku 30, Kulia ni mbunge wa Kasulu Mjini Mhe.Moses Machali Mbunge wa Kasuluu Mjini, Mwenye shati la Kijani ni Meja mstaafu wa JWTZ Clemence Ndayeza Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kasulu

Naibu waziri wa wizara ya nishati na madini Bw. Steven Masele ametoa siku 30 kwa shirika la umeme Tanzania TANESCO mkoani Kigoma kuhakikisha wateja wote waliolipia huduma hiyo wilayani Kasulu kufungiwa umeme vinginevyo hatua kali za kisheria na utumishi zitachukuliwa dhidi yao.
Akikagua mitambo ya kufua umeme pamoja na mradi mzima wa usambazaji wa umeme wilayani Kasulu, Masele amebaini kuwepo kwa makosa mengi ya kiutendaji na kiufundi na hivyo kufikia azimio hilo la kuwachukulia hatua kama hawatatekeleza agizo hilo

Mheshimiwa Masele ameagiza pia wananchi wa wilaya za Kasulu na Kibondo ambao hawajapata huduma ya umeme kwenda ofisi za TANESCO kulipia gharama za kuunganishiwa umeme (service line) na kwamba watakaopata tatizo watoe taarifa kwake

Aidha Mheshimiwa Masele ametoa namba yake ya simu kwa wananchi wa kasulu kwa malengo kuwa, endapo watapata taizo lolote la huduma ya umeme dhidi ya watumishi wa kampuni ya NEMES inayofanya kazi ya ujenzi wa miundombinu pamoja na Tanesco wenyewe wampigie simu ili achukue hatua
Katika malalamiko ya wananchi, wamemweleza Naibu waziri wa Nishati na madini Bw. Masele kuwa watumishi wa TANESCO pamoja na kampuni inayojenga miundombinu ya umeme katika wilaya ya Kasulu, kwamba ni waomba rushwa, wavivu na wazembe katika kukamilisha mradi huo
Mitambo miwili ya kuzalisha umeme iliyofungwa wilayani Kasulu inauwezo wa kutoa umeme wa MEGAWATT 2.5 lakini hadi sasa umeme unaotumika tangu kuwashwa kwa mitambo hiyo ni megawatt 04 pekee kitendo ambacho ni hasara kwa shirika la umeme kutokana na gharama za uzalishaji kutolingana na wateja (kipato)

Wilaya za Kasulu na Kibondo zimepata umeme wa generator unaozalishwa na TANESCO kwa mara ya kwanza tangu Tanganyika kupata uhuru, pamoja na hayo ujio wa huduma hiyo umeleta changamoto mpya ya rushwa na ufisadi miongoni mwa watumishi wa umma.

No comments: