Monday, August 27, 2012

ARCADO NTAGAZWA WAZIRI WA ZAMANI NA KAULI ZA KUTATANISHA


 

Arcado Denis Ntagazwa ni mmoja wa wasomi wa enzi hizo ambaye akitokea kijiji cha KIzazi wilayani Kibondo mkoani Kigoma alifanikiwa kushika nyadhifa nyingi ikiwemoo ubunge na uwaziri kwa nyakati tofauti tangu wakati wa Rais wa kwanza wa Tanzania hayati baba wa taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere

Ntagazwa ambaye amewahi kujinadi kama mbunge wa kudumu wa jimbo la Muhambwe aliangushwa na mwana usalama wa Ikulu Felix Ntibenda katika kinyang’anyiro cha Ubunge katika kura za maoni ndani ya CCM

Haikuwa jambo jepesi kumng’oa Ntagazwa kwani alikuwa amejizatiti vilivyo kwa kuwaweka sawa vijana, wanawake na wazee waliokuwa wamelishwa yamini kwa Khanga, Baiskeli na simu za mkononi alizowagawia kuwashawishi wamwamini kuwa ndiye anayefaa kuwa mbunge kwa miaka mingine 5 atimize miaka 30 ya ubunge

Leo Ntagazwa ni kamanda wa CHADEMA amekuwa akizunguka huku na kule kukinanga chama chake cha zamani CCM akiwatuhumu kuwa nii vinala wa Rushwa na wanadidimiza maendeleo

Ntagazwa hakukurupuka kwenda CHADEMA, kutokana na umakini na ufahamu wake alijipa muda wa kutafakari tangu mwaka 2005 hadi 2010 alipojaribu tena kugombea katika kura za maoni za CCM na kushindwa

Je?  anapopambana leo na CCM kwa tuhuma za RUSHWA ni dhamira ya dhati au HASIRA ZA KUUKOSA UBUNGE ndani ya CCM na hata huko chadema alikokwenda baadaye

Wanaharakati hasa vijana tunapaswa kujiridhisha na DHAMIRA ya NTAGAZWA na tujiulize pia kama yeye hakuwa mtoa rushwa kabla ya kuhujumiwa na wapiga kura waliokula vya kwake na kasha kumtosa katika karatasi za kura

Hizi siasa za watanzania wanaokuwa watakatifu mara wanapokosa nafasi CCM na kuhamia upinzani huku wakituaminisha kuwa wao ni wema na wanayajua madhambi ya zamani nadhani ni busara kama wakitanguliza kuomba radhi kwa maovu waliyafanya kabla ya kututangazia utakatifu wao baada ya kuhama CCM

Huo ndio uungwana na sisi tutawaamini

 

Haya ni Maoni yangu ninakaribisha mjadala katika hili

0764243377

No comments: