Monday, August 27, 2012

WAANDISHI WA HABARI MSIGEUZWE KUWA MABANGO


Mhariri mtendaji wa gazeti la JAMHURI Bw. Deodatus Balile amebainisha kutofurahishwa na tabia ya ngwaandishi wengi nchini kugeuzwa kuwa mabango ya makampuni na taasisi mbalimbali kwa kuvaa mavazi hususani fulana (tshirt) zenye matangazo

Balile amesema hayo mjini Kigoma wakati wa mafunzo ya maadili kwa waandishi wa habari mkoani humo sambamba na kufafanua azimio la Dar es salaam juu ya UHURU WA UHARIRI NA UWAJIBIKAJI yanayosimamiwa na Barala la Habari Tanzania MCT

Ameeleza kuwa maeneo mengi hususani mikoani waandishi wa habari wengi wamekuwa wakivaa kila e matangazo ya makampuni Fulani, jambo ambalo tafsri yake ni kwamba habari nyingi zinazoandikwa na waandishi hao ni zile zilizogharimiwa na mashirika, kampuni au taasisi iliyomgwia fulana au kofia.

“jamani vaeni mavani yenu tena yawe ya heshima, si kuvaa nguo za kupewa, kwani ninyi hamuwezi kujinunulia nguo? Hta hivyo nawapongza Kigoma hamna tabia hiyo ya kuguzwa kuwa mabango ya makampuni na mashirika kwa kuvaa mavazi yao” alisema Balileoni
Tanzania ni miongoni mwa nchi chini ya jangwa la sahara ambazo waandishi wake wa habari wanaishi kwa kipato cha chini sana kutokana na wamiliki wa vyombo vya habari kutowapa mikataba na pia kuwalipa kiwango kidogo cha mishahara au posho za kazi zao
kwa waandishi wa mikoani hasa wanaoandika habari za magazeti, wengi wao hawapati malipo kutoka kwa vyobo vyao na hivyo maisha yao huyaendesha kwa kutegemea posho kutoka kwa wadau wa habari, mashirika na taasisi mbalimbali za serikali, pindi wanapokuwa na jambo la kuandikwa au kutangazwa na vyombo vya habari hulazimika kutoa chochote (mshiko) ili habari zao ziandikwe
Jambo hili linachangia sana kuporomoka kwa maadili ya uandishi wa habari na vyobo vya habari.

No comments: