Na. Everister Lucas
Singida Tanzania
“Hawa nao wanaongea nini? Mie wala hawatanihesabu kabisaaa;
tena wakome waishie huko huko kwangu hata wasije. Tena zoezi lenyewe linaanza
usiku! Hawapati mtu.” Nilimsikia rafiki yangu akibwabwaja huku kakodolea macho
kioo cha Runinga; Nikamuuliza kulikoni mbona alikuwa akiiongea peke yake?
Baadae kidogo nilibaini kuwa katika kipindi cha jambo leo
cha TBC 1 ambacho kilikuwa hewani walikuwa wakitoa mada juu ya zoezi zima la sensa ya watu na
makazi na jinsi zoezi hilo
litakavyofanyika. Hali hii ilinifanya nimuulize shoga yangu huyo ni nini
asichokijua kuhusu sensa. Nae akanambia kuwa haoni umuhimu wa kuhebiwa na kudai
kuwa huo ni usumbufu.
Hili likanirudisha nyuma na kunikumbusha kikao cha hivi
karibuni kati ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone na viongozi wa
madhehebu ya dini hapa mkoani Singida juu ya sensa ya watu na makazi
inayotarajiwa kufanyika nchini pote usiku wa kuamkia Agosti26 mwaka huu na
kudumu kwa muda wa siku sabana, akisisitiza kuwa watakaohesabiwa ni wale wote
watakaokuwa wamelala katika kaya yoyote nchini Tanzania usiku wa kuamkia tarehe
hiyo.
Tumesikia vyombo mbali mbali vya Habari vikiripoti juu ya
changamoto zinazojitokeza katika zoezi zima la sensa kwa imani potofu au kwa
kutokujua umuhimu wa zoezi hili.
Kuna baadhi ya watu pia wanasambaza ujumbe kwa njia ya
vipeperushi na ujumbe mfupi wa maneno wa simu kuwashawishi wasijitokeze
kuhesabiwa.
Na hili lilidhihirishwa na Dk. Kone huku akisoma kivuli cha
habari iliyochapishwa na wanaharakati wa dini ya Kiislamu na kutolewa katika
gazeti la raia mwema likiwahamasisha waislamu kutoshoiriki katika sensa.
Akiendelea kusoma ujumbe huo ambao unatuhumu kuwa toka enzi
za ukoloni idadi ya waislamu ilikuwa ni asilimia sitini lakini kadiri sensa
inavyoendelea idadi hiyo inazidi kupungu.
Hata hivyo kutokana na uzito wa suala hili; ilimlazimu Kone
kuwataka maafisa wa usalama waliohudhuria kikao hicho kulifuatilia suala hili
kwa ukaribu hata kumpata muhusika ili hatua za kisheria zichukuliwe juu yake.
Kwa upande wao viongozi wa dini ya Kiislamu wakionesha wazi
kusikitishwa kwao na ujumbe huo, kwa nyakati tofauti tofauti walikemea vikali
kitendo hicho na kuahidi kuendelea na hamasa zaidi kwa waumini wao juu ya
umuhimu wa sensa.
“Zoezi la kuhesabu lilikuwepo toka enzi za Mtume
Mohamad(S.A.W) ambapo viongozi walitakiwa kupata idadi kamili ya Waislamu
kwaajili ya kufanya mipango ya maendeleo.” Shekhe Issah Nassor.
Shekhe Issah alizidi kufafanua kuwa haoni tatizo juu ya
zoezi hilo kwa
vile ni agizo pia kutoka kwa Mungu na pia ni kwa maendeleo ya nchi. Pia
alisisitiza kuwa yeye binafsi yuko kwenye ziara za uhamasishaji juu ya sensa ya
watu na makazi na kumuahidi Kone kuwa na amani na zoezi litafanikiwa.
Kwa upande wa viongozi wa dini ya Kikristo hawakusita
kupongeza viongozi w enzao wad ii ya Kiislamu kwa kitendo cha ujasiri
walichokionesha kwa kulikemea wawzi wazi kundi hilo la wanaharakati wanaotaka kuvuruga zoezi
la sensa. Mwakilishi kutoka kanisa la sabato pia alisisitiza kuwa sensa
ilikuwepo toka enzi za kuzaliwa kwake Yesu Kristo ambapo Yuda aliamuru watu
wahesabiwe.
“ Tunachokifanya ni kile ambacho pia kipo katika maandiko
matakatifu. Ninyi ni walimu wazuri na mnakubalika katika jamii. Mimi nadhani
sijawatwisha mzigo mzito kwakuwa mmesema kuwa sensa ni sheria na ni amri.”Kone
No comments:
Post a Comment