Monday, August 27, 2012

MGOGORO WA MPAKA KATI YA TANZANIA NA MALAWI HALI TETE

Na. Prosper Kwigize

Baada ya mazungumzo kati ya Malawi na Tanzania kuhusu mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa kugonga mwamba, Tanzania imesema mazungumzo mengine yatafanyika tarehe 10 mwezi ujao kujaribu tena kutatua mzozo uliopo.
     
Katika mazungumzo yaliofanyika nchini Malawi mjini Mzuzu, Malawi ilitaka mzozo huo utatuliwe katika mahakama ya kimataifa ya ICJ.

Kwa upande wake Tanzania imepinga suaa hilo kutatuliwa na mahakama ya kimataifa badala yake kuwepo na mazungumzo zaidi

Hata hivyo serikali ya tanzania imeendelea na msimamo wake wa kupiga marufuku shughuli za utafiti wa mafuta zinazoendeshwa na Malawi

Hofu bado imetanda juu ya uwezekano mkubwa wa kuibuka kwa vita kali ya kugombania mpaka kama ilivyokuwa kwa Idd Amin Dada mwaka 1978

Nchi ya Malawi imelimega ziwa lote na kulifanya kuwa ndilo mpaka wa nchi zetu lakini haikufanya hivyo kwa upande wa Msumbiji ambao wao wanagawana ziwa hilo katikati

inakuwaje tanzania ihujumiwe kuwa ziwa lote ni la malawi lakini haifanyi hivyo kwa Mozambique?

angalia ramani hizi

 
Hii ni ramani inayoonesha mipaka ya Tanzania na nchi jirani kama ilivyochorwa tangu mwaka 1913, eneo la Ziwa Nyasa ambalo leo Malawi wanaliita Ziwa Malawi mpaka wa Tanzania na Malawi uko katikati ya ziwa, lakini malawi walibadili mpaka huo
 
 Ramani hii inaonesha sehemu ya ziwa Nyansa kama ilivyobadilishwa na Malawi miaka ya 1964 baada ya uhuru wa Taifa lao, eneo la ziwa linaiondoa Tanzania katika umiliki wa sehemu wa Ziwa hilo lakini ukitazama kwa chini eneo la Mozambique kitendo hicho hakikufanyika, wao wanagawana ziwa hilo katikati, Je ni nini hoja ya Malawi kwa Tanzania?
 
let us discuss

 

No comments: