Na, Doris Meghji
Singida
Wasimamizi na
makarani wote wa sensa ya watu na makazi wilayani Manyoni wametakiwa kuzingatia
maadili ya kazi,ushrikiano wa karibu kati ya wasimamizi, makarani na viongozi
wa ngazi zote ikiwa ni pamoja na kujiepusha na masuala ya ushabiki wa kisiasa
na kidini kwani takwimu zitakazokusanywa zitatumika kwa ajili ya maendeleo na
sio vinginevyo
Bi Toufiq
“ushirikiano wa karibu (team work) ni muhimu kati ya wasimamizi,makarani na
viongozi wa ngazi zote ni muhimu katika kufanikisha zoezi hili” alisisitiza
Mkuu wa wilaya huyo.
Hata hata hivyo
amewataka kuacha mahusiano yatakayohatarisha utendaji kazi ikiwa ni pamoja na
suala la kujihusisha na ushabiki wa kisiasa na kidini kwani takwimu
zitakazokusanywa zitatumika kwa ajili ya shughuli za maendeleo na sio
vinginevyo
Suala la kuwa
namikini na vyombo vya habari halikusahaulika ambapo Bi Fatma Toufiq amewataka
wasimamizi na makaraini hao kuwa makini na vyombo hivyo kwani msemaji mkuu wa
masuala ya sensa katika wilaya ni mkuu wa wilaya au Mratibu wa Sensa wa wilaya
tu.
Hivyo amewataka
washiriki wa mafunzo hayo kutumia fursa hiyo ya mafunzo kuzingatia kwa makini
mambo yote wanayofundishwa na wakufunzi wakati wote wa kipindi cha mafunzo kwa
kuzingatia umuhimu wa kipekee wa sense ya mwaka huu ambapo takwimu zake
zitatumika kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa malengo ya millennia ya
mwaka 2015 na program mbali mbali za maendeleo nchini
Mwisho
No comments:
Post a Comment