Wednesday, August 15, 2012

WAKIMBIZI KUTOKA KENYA WAHIFADHIWA TANZANIA


Wakati dunia akiamini kuwa hali ya kisiasa na kikabila nchini Kenya imetulia baada ya kuwepo kwa mwafaka wa kisiasa baina ya makundi na vyama hasimu nchini humo, familia moja ya watu watano kutoka Kenya wako nchini Tanzania wakiomba hifadhi ya ukimbizi



Wakimbizi hao walikimbia nchi yao tangu mwaka 2010 kutoka Kenya kupitia Kampala Uganda na kufanikiwa kuingia nchian tanzania ambapo wanataja kuwa waliishi kama wakimbizi jijini Dar es salaam



Kwa sasa familia hiyo inaishi nje bila hema wala banda la kujihifadhi katika kambi ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walioko Nyaruigusu mkoani Kigoma nchini Tanzania



Wakiongea kwa machungu makubwa wakenya hao wamebainisha kuwa wanalazimika kulala nje kufuatia unyanyasaji wanaofanyiawa na wakimbizi wenzao kutoka DRC, Rwanda na Somalia wanaoomba hifadhi nchini tanzania ambao kwa sasa wanahifadhiwa ndani ya kambi ya wakimbizi wa DRC wilayani Kasulu.



Daniel g’ang’a na mama yake Lucy Wambui wanaelezea kilichowasibu hai kulazimika kuwa wakimbizi nchini Tanzania na maisha yao kwa sasa



Akitoa maelezo juu ya uwepo wa Wakenya hao nchini tanzania na taratibu zainazochukuliwa na serikali ya Tanzania mkuu wa idara ya wakimbizi ya wizara ya mambo ya ndani ya Tanzania wilayani Kasulu Bw. Fredrick Nisajile ameeleza kuwa kamati ya taifa ya utambuzi na utoaji hadhi ya ukimbizi inalifanyia kazi jambo hilo



Hata hivyo hakuwa tayari kuelezea kuhusu malalamiko ya huduma duni wanazopata kambini humo kutokana na kutokuwepo ofisini kikazi na kuahidi kulitolea ufafanuzi baadaye



Sirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR wilayani Kasulu limekataa kutoa maelezo kwa kile kinachotajwa kuwa ofisi hiyo haina mamlaka ya kuzungumza na vyombo vya habari hadi kibali kutoka Dar es laam



Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu nchini tanzania kwa sasa inahifadhi wakimbizi wapatao 66 elfu na kati yao wamo wakimbizi kutoka DRC ambao ndio wengi, pia wamo wakimbizi kutoka Burundi na Rwanda



By. Prosper Laurnt Kwigize, channel Afrika Tanzania

No comments: