Br. Welhard Mukesha ambaye ni mkuu wa kituo cha afya ya akili kinachomilikiwa na shirika la Brothers of Charity Marumba mkoani Kigoma akiwa katika moja ya majukumu yake ya kutoa huduma za afya ya akili kwa wagonjwa
Na. Prosper Kwigize
Magonjwa ya akili ni moja ya changamoto zinazolikabilii bara
letu la afrika na hivyo kuchangia kuzorota kwa maendeleo ya jamii na hasa kaya
zenye wagonjwa wa akili
Kwa mujibu wa Takwimu za Kanisa Katoliki nchini Tanzania zaidi ya wagonjwa 68,000 wamepatiwa huduma za afya ya akili katika kituo cha shiopokelewa rika la kitume la Brothers of Charity kilichoko Marumba mkoani Kigoma ambapo 25,000 kati yao ni wagonjwa waliolazwa na kisha kuruhusiwa baada ya akili zao kupata nafuu
Aidha jumla ya wagonjwa wa akili 43000 wamepata huduma kwa nyakati tofauti wakitokea nyumbani ambapo ama wanakuja na kupewa dawa na maelekezo ya matumizi wakiwa majumbani mwao
Hata hivyo Br. Welhard Mukesha ambaye ni mkuu wa kitengo cha tiba ya afya ya akili Marumba anafafanua kuwa, kutokana na changamoto mbalimbali jumla ya wagonjwa wa akili 24 wanalazimika kuishi maisha yao yote katika kituo cha Marumba
Br. Mukesha anabainisha kuwa wagonjwa hao wataishi kituoni hapo kutokana na ama kutengwa na jamii, kutokuwa na ndugu wa kuwalinda na kuwapa huduma za kijamii pamoja na wengine kuwa na ugonjwa sugu wa akilii ambao ulitokana na kucheleweshwa kupata huduma ya matibabu.
Jamii imekuwa na mitazamo tofauti kuhusu magonjwa ya akili hali inayosababisha mikakati ya kupambana na magonjwa hayo ikiwa ni pamoja na vyanzo vyake kushindikana kuzuiliwa kikamilifu na hivyo jamii kuendelea kuathirika.
Moja ya sabau zinazotajwa kuchangia kuwepo kwa magonjwa na
wagonjwa wa akili ni matumizi ya madawa ya kulevya na ulevi wa pombe za
kupindukia hususani pombe za kienyeji na zile za viwandani maarufu kama Viloba
n.k
Ipo hoja pia kuwa magonjwa ya akili chanzo chake ni Kurogwa
au kurithi kutoka kwa wazazi au ndugu yeyote katika ukoo
Ssehemu kubwa ya jamii imekuwa ikikimbilia kwa waganga wa
jadi kwa ajili ya kutafuta tiba ya magonjwa ya akili lakini kwa bahati mbaya ni
wachache wanaopona hususani wale wanaopata ugonjwa huo kutokana na matatizo ya
kisaikolojia na matumiziz ya madwaya ya kulevya au ulevi wa pombe kupindukia
Ukosekanaji wa vituo vingi vya tiba ya akili yaweza kuwa
chanzo cha kudumu na kuendelea kuwepo kwa dhana potofu ya waganga wa jadi na
kuendelea kuzagaa kwa vijana wengi wa kike na wakiume katika mitaa wakiwa
wagonjwa na wahanga wa matatizo ya afya ya akili barani afrika
Shirika la Kidini la Brothers Of Charity la Kanisa katoliki
limeanzisha kituo cha afya ya akili mkoani Kigoma na tayari wagonjwa wengi
wamepata tiba na wengine wanaendelea kupata huduma hiyo na kupona. Inaelezwa kuwa
wakati mwingine si wote wanaohitaji kupatiwa madawa bali ushauri nasaha,
kupumzishwa kwa muda na kuwapa shughuli ndogondogo kunawawezesha akili yaoo
kuwa vizuri na hatimae kurejea katika afya yao ya kawaida
Pichani ni Bw. Mathias Richard mwenye umri wa miaka 32 ni
mmoja wa wagonjwa wa akili wanaopatiwa matibabu katika kituo cha Brothers of
Charity Marumba mkoani Kigoma- yeye anakili kuwa kama asingeletwa katika kituo
hicho angekuwa barabarani akifanya matendo ya wehu na wendawazimu
Picha ya pilii ni Bw. Salila Josephat Msigwa, mwenye umri wa
miaka 36, yeye anamuuguza ndugu yake ambaye baada ya kutangatanga kwa waganga
wa jadi aliamua kumpeleka katika kituo cha afya ya akil Marumba; sasa anakili
kuwa ni vijana wengi wenye matatizo ya akili lakini hawajafikishwa kwenye vituo
vya tiba. Msigwa anadai pia kuwa wengi wa wenye matatizo ya afya ya akili
chanzo kikibwa ni matumizi ya madawa ya kulevya, bangi na pombe kali, ingawa
anakubali pia kuwepo kwa magonjwa ya kurithi pamoja na kurogwa.
PICHA 3. Bw. Nicolaus Edward muugizi wa kituo cha afya ya
akili Mrumba mkoani Kigoma, yeye anakil kuwa wengi wa wagonjwa wanaopokelewa
katika kituo chao ni vijana wanaotumia madawa ya kulevya hususani Bangi pamoja VILOBA,
aidha hisia ya kurogwa ipo na kwamba haina ukweli kwa kiasi kikubwa, anakili
pia kuwa yapo matatizo ya akili yanayotokana na urithi na kwamba tatizo kubwa
lililopo ni jamii kutowapeleka katika vituo vya afya kupata tiba ba badala yake
kuwaacha wakizagaa mitaani.
No comments:
Post a Comment