Mkuu wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida Bibi Fatuma Toufiq akitembelea moja ya kaya wakati za zoezi la sensa
Doris Meghji Jumatatu
Manyoni – Singida
Zoezi la sensa ya watu na makazi
wilayani Manyoni linaendelea vizuri licha ya changamoto mbali mbali
zilizojotokeza kwenye utekelezaji wa zoezi hilo katika baadhi ya vitongoji na
vijiji juu ya suala la mipaka kati wilaya ya Uyui, Bahi,Sikonge na Manyoni
Mkuu wa wilaya ya Manyoni Bi Fatuma
Toufiq ametoa taarifa hiyo wilayani humo jana mara baada ya kutembelea baadhi
ya maeneo na kujua hali ya zoezi hilo limekwendaje
Bi Toufiq amesema kuhusu suala la
mipaka katika vijiji vilivyoko mpakani kati ya wilaya yake na wilaya za
Uyui,Bahi na Ikungu limetatuliwa kwa vijiji hivyo kuhesabiwa kuwa viko manyoni
kutokana na ramani za kuhesabia maeneo (EA) zinavyoonyesha kwa makarani wa
sensa ya watu na makazi wilayani humo
Aidha amesema katika wilaya yake
wananchi wengi wameitikia zeozi hilo kwa kutoa ushrikiano kwa makarani wa sensa
ya watu na makazi wa madodoso yote kwa kutoa taarifa sahihi kwa makarani huku
akiwataka wananchi kutohujumu zoezhi hilo kwa kutoa ushrikiano kwa makarani wa
sensa
Amesema “Ni kaya mmoja nilivyopewa
taarifa kuna mtu alikataa kuhesabiwa akidai yeye ni muislam,lakini baada ya
kuelimishwa na karani wetu alikubali kuhesabiwa kwa hiyo mwandishi hilo ni kaya
moja ambayo alijitokeza mtu asiyetaka kuhesabiwa na kutatuliwa” alisema Mkuu
huyo.
Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya
amesisitiza wananchi kuendelea kutoa ushrikiano kwa makarani hao wa sensa ili
kufanikisha zoezi hilo la sensa ya watu na makazi litakalodumu kwa muda wa siku
saba huku wilaya hiyo ikiwa na jumla ya kata thelathini.
Mwisho
No comments:
Post a Comment