Wednesday, August 8, 2012

UCHUMI DUNI MKOANI SINGIDA

Na, Doris Meghji
Singida

Tatizo la mtaji ndogo na masoko ndani na nje ya mkoa wa singida wa  bidhaa  za wajasiliamali  kwa wanachama wa shirika lisilo la kisekali la kanisa  katoliki liitwalo KOLPING  parokia ya Singida  limekuwa likiwakumba wajasiliamali hao nakukwamisha lengo lao la kujikwamua kiuchumi

Akiongea na Kiongozi katika ofisi ya familia ya Kolping mara baada ya misa takatifu, Mwenyekiti wa shirika hilo parokia ya Singida Bi Mary Ngure amelezea juu ya changamoto mbali mbali zinazowakabili  ikiwa ni pamoja na kukusa masoko ya kuuzia bidhaa  wanazozalisha ndani na nje ya mkoa wa singida hali inayorudisha nyuma hari ya uzalishaji mali wa bidhaa hizo.

Aidha suala la mtaji likiwa ni changamoto kubwa kwao linalowakwamisha kununua vifungashio vya bidhaa zao inayowakwamisha hata kushirika katika maonyesho mbali mbali ya biashara wanapopata fursa amesisitiza Mwenyekiti huyo

Naye mratibu wa Kolping jimbo la singida Bwana Richard Assey alisema kutokana na changamoto hizo kolping itasaidia kuwatafutia masoko ndani na nje ya mkoa wa singida na kuoendelea kuwajengea uwezo na kuongezea  ujuzi katika usindikaji wa karanga na utengezeji wa mvinyo kwa kutumia maua ya rozela zikiwa ni mali ghafi zinazopatika katika maeneo yao

Hata hivyo katika kuteleza azma na lengo la mwasisi wa shirika hilo la Adolf  Kolping la watu kuondokana na umaskini kwa kufanya kazi pamoja na sala jumla familia arobaini na tatu  zimepatiwa mafunzo mbali mbali ya ujasiliamali katika utengenezaji wa sabuni,batiki,shampoo na unga wa lishe ikiwa ni miongoni mwa ujuzi juu ya bidhaa walizojifunza kutengeneza.

No comments: