Na Evarista Lucas
Singida
Uongozi wa Klabu ya Waandishi wa
habri Singida(SINGPRESS); imeuomba uongozi wa Klabu ya waandishi wa habari
Kagera kuwa mtandao wa mahusiano ambao
utasaidia katika kubadilishana mawazo haswa kwa upande wa kiutendaji.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya
kuagana iliyofanyika katika eneo la Bukoba Pub kati ya wajumbe kutoka Singida
na baadhi wanachama wa KPC; mwenyekiti wa SINGPRESS Bwana Seif Takaza alisema ,
“Mimi naona tusiishie hapa tu bali tuunde mtandao wa mahusiano kati yetu na
ninyi wanaKagera. Natumaini kuwa mtandao huu utaleta mabadiliko makubwa sana na
kuwa mfano wa kuigwa na Klabu zingine.”
Ziara hii ni utekelezaji wa mpango
mkakati uliowekwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) katika
mkataba uliotiwa saini na viongozi wa Klabu wanachama ambapo pia wanachama
wamekuwa wakinufaika na mafunzo mbali mbali yanayoendelea kutolewa na UTPC.
Katika ziara hiyo ya siku tatu iliyowajumuisha viongozi watatu
na wanachama watatu wa SINGPRESS ; wajumbe hao walipata fursa ya kubadilishana
uzoefu wa kiutendaji kupitia mahojiano ya hapa na pale na kubwa zaidi wajumbe hawa walipenda kujua
kuhusu vyanzo vya mapato vya KPC.
“Sisi tuna mradi wa
steshenari(kutoa kopi) ambao unatuingizia kiasi cha shilingi laki moja na
ishirini kwa mwezi. Pia tumeshawahi kuomba miradi mbali mbali huko nyuma na
tukapata shilingi ukiwemo mraadi uliohusu kuripoti mambo ya sheria na jinsi ya
kuripoti kesi za rushwa ambapo mradi huo uligharimu kiasi cha shilingui milioni
ishirini na saba za Kitanzania kutoka tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa
Tanzania(TAKUKURU) na pia mfuko wa kusaidia jamii(The Foundation for Civil
Society).” Alisema Mwenyekiti wa KPC
Bwana John Rwekanika.
Rwekanika alifafanua kuwa kwa
upande wao wameunda kamati ndogo ya miradi ambayo kazi yao kubwa ni kubuni
miradi na kuiwasilisha katika kamati ya utendaji amabapo inabarikiwa. Pia Bwana
Rwekanika alieleza kuwa wajumbe wa kamati hiyo wamekuwa wakipata asilimia
kidogo kutoka kwenye miradi wanayoipata ikiwa nikuwatia moyo wa kuendelea na
shughuli hiyo.
Naye katibu mtendaji wa SINGPRESS
Bwana Abby Nkungu alitaka kufahamu
mikakati waliojiwekea KPC
kuepukana na na utegemezi wa UTPC. “Tuko
mbioni tunataka kujenga jingo la kibiashara ambalo litasaidia
kutuingizia kipato ni adha kubwa kukaa unaomba omba.” Alisisitiza Rwekanika
Kwa upande wake katibu mtendaji wa
KPC BwanaPhinias Bashaya alisema; “ Mwaka
juzi tuliendesha mradi wa
shilingi milioni arobaini na mbili
kuhusu suala la wananchi kutokujitokeza kupiga kura. Katika kradi huo
pia tuliokoa kiasi cha fedha ambacho kilitusaidia kununua mashine ya
kuburuza(fotokopi).
Kwa upande wao wanachama wa
SINGPRESS(waliokuwa katika ziara hiyo) wameipongeza KPC kwa uataratibu mzuri
waliojiwekea katika suala zima la utendaji na pia kuimarisha mahusiano kati yao
na wadau wa habri mkoani hapo.
“Tunajitahidi kupunguza migogoro
kati yetu na wadau haswa linapokuja
suala la mialiko.” Alisema Mwekahazina wa KPC BibiL ilian Lugakingira na
kuongeza kusema kuwa migogoro kati ya wadau na waandishi wa habari iantokea
sana kwenye mialiko kwahiyo wanakuwa
makini sana kuchagua waandishi makini ili kuepusha migogoro.
No comments:
Post a Comment