Mwenyekiti wa ccm Mkoa Jorum Alute akiwa na Mwenyekiti wa UWT wilaya Bi Yagi Kiaratu na pembeni yake ni msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Bi Queen Mulozi mkuu wa wilaya ya Singida.
Na. Doris Meghji
Singida
Zikiwa chaguzi
mbali mbali za jumuhiya za chama cha mapinduzi ngazi za wilaya mkoani singida
zimekamilika kufanyika wanachama wa jumuhiyia hizo wametakiwa kuchagua viongozi
makini na wenye uwezo wa kuongoza ili kuhakikisha chama cha mapinduzi
kinaendelea kushika dola
Mwenyekiti wa
chama cha Mapinduzi mkoa wa Singida Bwana Jorum Alute ametoa rai hiyo mapema
wiki hiki wakati akifungua mikutano mikuu ya chaguzi za jumuhiya hizo kwa
kuaasa wanachama kuchagua viongozi watakao kuwa tayari kufa kwa ajili ya
kukipigania chama cha mapinduzi ili kiendelee kushika dola hivyo viongozi
watakao chagua kwenye chaguzi hizo wawe viongozi bora na makini watakao
kikisaidia chama hicho kuendelea kushika dola kupitia mafiga yake matatu ambayo
ni UVCCM, UWT na
WAZAZI.
“viongozi mtakao
wachagua watuhakikishie ushindi wa chaguzi za serikali za mitaa mwaka 2014 na
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,hapa mjini tumeingiliwa na vyama vya upinzani kila
mtu anafahamuzi,mtakao tuokoa ni ninyi, ni uchaguzi huu wa leo,mtachagua
viongozi ambao wako tayari kufa na kupona kuhakikisha chama cha mapinduzi ili
tuendelee kushika dola.Singida mjini mmchoka na amani tulionayo? Alisitiza kwa
swali mwenyekiti Alute
Aidha alisitiza
juu ya suala la umoja wa kitaifa ulioachwa na Baba wa Taifa mwalimu Julius
Kambarage Nyerere, Mwenyekiti huyo wa CCm mkoa wa Singida anasema “ Baba wa
taifa alituachia umoja na mshikamano, umoja wa kitaifa bila kujali wewe ni
rangi gani kabila gani na dini gani aliunda taifa la umoja wa kitaifa nchini
Tanzania unaweza kuishi mahala popote na hakuna atakaye kuuliza wewe ni kabila
gani na wenyeji wakukaribisha bila shida yoyote.
Sasa taifa limeanza
kumeguka meguka watu wameanza kuingiza udini wameanza kuingiza umajimbo
wanataka wakitawala wao warudishe majibo ambayo yalikuwa ya ukoloni lakini
wanataka wao sasa ni kwamba warudishe majimbo kwa maana ni kwamba unarudisha
ukabila kama mkuu wa mkoa awe mnyaturu au mnyiramba,kama ni mkuu
wa wilaya awe mnyaturu au mnyiramba na wanataka hayo majimbo au
kila mkoa mkoa uwe na wabunge wake lake na mipango ya maendeleo yatokane na
rasilimali za mkoa wetu wa singida kwa sababau wao tayari wameshaendelea wanarasilimali
zaidi kuliko sisi wana madini,wana mlima Kilimanjaro,wana kahawa wana mazao ya
kudumu ambayo wanawaletea maendeleo
Hao sio watu wa
kuaachia taifa hili” alisisitiza Mwenyekiti Alute
Hivyo aliwataka
washikamane wachague viongozi bora na sio viongozi
Hata hivyo katika
changuzi hizo kwa upande wa uchaguzi wa UWT wilaya ya singida mjini aliyeshinda
nafasi ya uenyekiti ni Bi Consolata Mziray alipata kura 184 kati ya kura 294
zilizopigwa huku akiwashinda wagomba wenzake ambao ni Hadija Simba aliyepata
kura 97 na Immaculata Ilanda Njiku mwenye kura 3 kati ya kura 274 zilizopigwa
Kwa upande wa
wagombea nafasi mkutano mkuu wa UWT taifa ambao ni Jane Kishari mwenye kura
203,Bi Marium Kambi aliyepata kura 187,Bi Scola Marwa kura 167,Bi Aisharose
Matembe kura 110, Bi Saidati Mziray Kura 42,Bi Hadija Simba kura 28, Bi Hamida
Saidi kura 21 Bi Mwanahasha Hamisi kura 16 huku Bi Pili Athumani alipata kura
12 kati ya kura 294 zilizopigwa katika mkutano huo na kuwafanya Bi Jane Kishari
mwenye kura 203,Bi Marium Kambi mwenye kura 187 na Bi Scola Marwa mwenye kura
167 kuwa wajumbe wa mkutano Mkuu wa UWT taifa kutoka jumuhiya hiyo wilaya ya
Singida Mjini.
No comments:
Post a Comment