Na Mwandishi Wetu
MUSOMA
CHAMA cha Waandishi wa Habari mkoani
Mara MRPC, kimemfukuza uanachama wa chama hicho, mwandishi wa habari wa radio
Free Afrika mkoani Mara Bw Maxmilian Ngesi baada ya kukiuka makubalino ya chama
hicho yaliyofikiwa juzi ya kutoandika kabisa habari za jeshi la polisi mkoani
humo.
Akizungumzia kufukuzwa kwa Mwandishi huyo mwenyekiti wa chama
hicho Bw Emmanuel Bwimbo,alisema kuwa Ngesi amekiuka makubaliano ya waandishi
wenzake na chama kwa ujumla baada ya kusikika akitangaza habari za jeshi la
polisi kwa kumkariri kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara.
“ Sisi kwa kauli
moja tumekubaliana kutofanya kazi na Jeshi la Polisi Mkoani Mara baada ya
Matukio kadhaa likiwemo ya kuuawa kwa mwandishi wa habari mkoani Iringa na
kutunyima kibali cha Maandamano yetu ya Amani kupinga Mauaji hayo” alisema Bw
Bwimbo
Bw Bwimbo alisema kuwa kitendo hicho kinaonyesha jinsi gani
mwandishi huyo alivyokiuka makubaliano ya pamoja na kuwasaliti wenzake ambao
wamekubaliana kwa pamoja kuwa hawataandika habari za jeshi hilo kutokana na
kuzuiwa waandishi kutoandamana katika maandamano ambayo yaliitishwa nchini kote
kulaani kitendo cha mauaji ya mwandishi wa kituo cha chanel Ten mkoani Iringa
Daud Mwangosi.
Alisema Ngesi kama mwanachama alitakiwa kutii maamuzi ya
chama na tamko la chama chake kwa vile tamko hilo limewataka wananchama wote na
siyo kwa mkoa wa Mara tu lakini pia baadhi ya mikoa imetoa matamko na misimamo
hiyo lakini cha kushangaza yeye amekaidi na kwenda kinyume.
Aidha
Mwenyekiti huyo alisema kamwe chama hicho hakiwezi kuvumilia mwandishi atakaye
kiuka agizo hilo na hatua ambayo imechukuliwa kwa Ngesi ni mfano kwa waandishi
wengine hadi hapo tamko hilo litakapo tenguliwa.
Jumatatu wiki hii
waandishi wa habari walifanya maandamano nchi nzima wakilaani mauaji ya
mwandishi mwenzao Daudi Mwangosi ambapo kwa mkoa wa Mara maandamano hayo
yaliuzuiwa na polisi hali iliyofanya chama cha waandishi wa habari kukataa
kuandika habari za jeshi hilo mkoani Mara.
No comments:
Post a Comment