Sunday, September 23, 2012

JIKWAMUE KIUCHUMI - MAKALA KUTOKA ARUSHA

 
Na:
Matinde  Nestory
Katika hali ya kawaida ujasiri ni ile hali ya uthubutu wa kuamua kuanzisha biashara, na ujasiri huo utakuletea faida katika biashara yako, na mali ni ile hali ya kuwa na uwezo wa kumiliki kitu mfano fedha,mifugo,bidhaa  pamoja na hayo naweza sema kuwa ujasiriamali ni ile hali ya kujiajiri mwenyewe bila ya kuwa na mkataba na mtu.
Nia ya kuandika makala hii ni kutaka mwananchi kujifunza ujasiriamali ambao utakupanua kimawazo,kimtazamo na hata kiakili,pamoja na hayo ujasiriamali utakusaidia kujua mbinu mbalimbali za kubuni biashara mpya,kupanua biashara au soko pamoja na huduma kwa wateja.
Mpenzi msomaji ukweli ni kwamba akili  za kuzaliwa hazitoshi katika kumwezesha mfanyabiashara wa leo kubuni na kuendesha biashara yenye mafanikio.Biashara yenye mafanikio ni biashara ambayo ni mathalani inaweza kuhimili ushindani wa soko huria pamoja na kukuwezesha kurudisha mkopo uliokopa kwa ajiri ya kuanzisha biashara.
Ndugu msomaji katika kubuni biashara mpya ni kwamba mfanyabiashara anatakiwa kubuni biashara ambayo itamletea mafanikio na sio kubuni biashara ambayo itamletea hasara japo katika biashara hasara hazikosekan,pia katika kubuni biashara mpya kinachohitajika ni mawazo yako ambayo yatakupelekea kubuni biashara nzuri ambayo itakuletea manufaa pamoja na kuweza kukua kiuchumi,pia wazo zuri la biashara litakusaidia kujua uzalishaji mali pamoja na kupanuka kimawazo na kiakili.
Katika kupanua biashara ukweli ni kwamba wakati huu ndio wa kufikiri zaidi kiubunufu na kimkakati na suala utakaloamua hapa ndilo litakalokusogeza mbele kibiashara utafiti unasema kuwa biashara nyingi hufa kabla ya kumaliza mwaka mmoja hii inatokana na kushindwa kumiliki ushindani wa kisoko unaosababishwa na wamiliki wa biashara husika kutokana na elimu ya ujasiriamali ambayo ingewawezesha kufanya maamuzi ya busara.
Pia biashara yoyote inatakiwa iwe pana hiini kutokana kuifanya biashara hiyo ijulikane sehemu mbalimbali mfano unaanzisha biashara ya batiki ili biashara hiyo ikue na kujulikana zaidi lazima uwe na vifaa vya kutosha ambavyo vitakusaidia katika kufanya biashara hiyo ikue kwa kuanzisha huduma mpya ndani ya biashara yako na katika sehemu mbalimbali za mkoa au kufungua tawi linguine ili kuipa nafasi biashara yako kufanya kazi katika wigo mpana zaidi.
Katika hatua ya kukomaa biashara inakuwa endelevu pamoja na vyanzo mbalimbali vya mapato vinavyoweza  kutengeneza faida inayoweza kutoshereza kubuni biashara nyingine mpya tofauti na uliyonayo pamoja na mafanikio hayo mwenye biashara anatakiwa asibweteke badala yake akae na mtandao wa taarifa ili kuifanya biashara mpya kila siku.
Hali kadhalika katika kuipanua biashara au soko mfanyabiashara unatakiwa kuongeza mtandao mfano kuongeza au kupanua soko lako ambapo hapo awali ulikuwa unafanya biashatra yako mkoani Arusha,Tanga,Shinyanga na sehemu nyingine.
Lengo la biashara ni kupata na kutunza wateja na si kupata fedha,ubora na ukubwa wa biashara unaangaliwa kwa wingi wa wateja wa biashara husika.Waswahili husema kuwa ghali kumpata mteja mpya kwenye biashara yako kuliko kumtunza au kuendelea kumfanya mteja wako wa zamani kuendelea kuwa mteja wako.Kwa mantiki hiyo ni kwamba changamoto za biashara za leo ni juu ya kupata wateja wapya kuliko kuendelea kumtunza mteja wa zamani lakini katika hali ya kushangaza si wafanyabiashara wengi wanajihusisha na mambo ya kutafuta wateja wapya bali wengi wanachojali ni pesa tu.
Pamoja na hayo wafanyabiashara wengi wa kitanzania wanafikiri biashara ni sehemu ya kuonyesha ufahari na majivuno bali biashara ni huduma kwa jamii nzima.Mwananchi hebu jiulize unakwenda kununua bidhaa Fulani unamkuta mtoa huduma au mmliki wa bidhaa hizo hana kauli nzuri je utaendelea kununua bidhaa zake ama utauliza na kwenda kwingine?ambako utapata bidhaa hizo kwa mhudumu ambaye anajua kanuni na sheria za mteja.
Mfanyabiashara yeyote mwenye busara atangalia faida ya mteja kwa mtazamo wa muda mrefu na sio mtazamo wa siku moja.Pia mfanyabiashara ambaye anajua wateja wake wanataka nini kwake uwa anapata wateja wengi tena wa kudumu kutokana na huduma yake anayotoa,hivyo mfanyabiashara yeyote anatakiwa awe na mbinu mbadala za kuweza kupata wateja ambao watadumu bila ya kuwapoteza ,wahenga walisema ni heri kupoteza bidhaa kuliko kumpoteza mteja ambaye anakuweka hapo kwa ajili ya kumhudumia.
Mwananchi amka jifunze ujasiriamali ambao utakusaidia kutatua matatizo ya kifamilia pamoja na kupata fedha ambazo zitakusaidia kukuza uchumi wa nchi na kujitoa katika janga hili la umasikini hivyo basi nakushauri acha kusema nimekosa kazi na huku akili umepewa za kufikiri.Hivyo basi ujasiriamali umewatoa watu katika hali duni na hivi sasa ni wafanyabiashara wa kimataifa,mwananchi unatakiwa uache uvivu fanya kazi ili kujikomboa katika janga hili la umasikini ambalo limekuwa tishio katika nchi.
Hata hivyo ujasiriamali ndio kiinua mgongo cha nchi,Ndugu msomaji hebu jiulize kama watu wote wangekuwa hawajishughulishi na biashara ya aina yoyote  je nchi hii ingeenda wapi pamoja na watu wangepata wapi mahitaji yao?Mwananchi amka jipange sasa hivi ni nyakati za kupambana kiume usiku na mchana fanya kazi sababu ukitegemea kuajiriwa serikalini utasubiri sana.hivyo jipange achana na dhana isemayo mie siwezi hakuna mtu katika dunia hiiasiyeweza kufanya kazi wote wanaweza kufanya kazi.
Pamoja na hayo waewza sema ujasiriamali ni ujasiri wa kutafuta mali na usifanya klazio kwa mazoea amka jipange na katika kujipanga neon kukata tama futa katika mawazo yako.
Mwisho  ningependa kukushauri ngugu msomaji wa makala hii jifunze ujasiriamali ambao utakutoa katika janga hili la umasikini na kuwa tegemezi na huku una mikono pamoja na macho,hivyo kumbuka siku zote ujinga ndio wa bei ghali zaidi kuliko bei ya elimu.

No comments: