NA Phesthow Sanga . Iramba
Mahakama Wilayani Iramba Mkoani wa Singida,Imepiga marufuku shughuli za Uchimbaji wa Madini Ya dhahabu katika Machimbo ya Sekenke wilayani humo kutokana na Eneo hilo kuwa na Mgogoro Mkubwa Ambao Umeshindikana kusuluhishwa na mkuu wa wilaya Yahya Nawanda .
Amuri hiyo halali Imetolewa jana na Hakimu mkuu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Mrisho K.Mrisho Baada ya kusikiliza kesi na, 10 ya mwaka 2012 iliyokuwa inahusu Zuio la Uchimbaji Madini, kati ya Mlalamikaji John Binner na Emmanuel Magai.
Kwa Mujibu wa hukumu iliyosomwa na hakimu huyo Ilieleza kuwa, Awali Emmanuel Magai alipeleka Ombi Mahakamani hapo kuomba Mahakama Imzuie John Binner kujihusisha na kutaka asilimia 20 ya mapato ya madini yanayopatikana mgodini hapo.
Aidha ilielezwa kuwa ,John Binner naye alipeleka Maombi Mahakamani hapo kumzuia Emmanuel Magai Kutoendelea na Uchimbaji kwa Sababu ameshindwa kumlipa Binner asilimia 20 mwenye Leseni halali na mmiliki wa Mgodi huo.
Hakimu Mrisho alitupilia mbali Ombi la Emmanuel Magai ,kwa kile alichodai kuwa lilikuwa na Mapungufu ,Alisema kwa upande wa John Binner vilele kulikuwa na mapungufu kadhaa hivyo Mahkama Inatoa Amri ya Mtu yeyote kutojihusisha na Uchimbaji kuanzia tarehe ya kusomwa hukumu hiyo jana.
Hakimu huyo Alisema kuwa, kwa kuwa ,Kesi mama Inaendelea katika Mahakama hiyo,hivyo wote watulie Mpaka Mahakama Itakapotoa Maamuzi kuwa mwenye Uhalali wa Eneo hilo ni nani; na hili Zuio ni la muda tu.
Kwa upande wake Emmanuel Magai, alisema kuwa Yeye ameridhika na Uamuzi wa Mahakama kwani Eneo lililotajwa ni la kijiji Cha Mgongo na si Eneo la kijiji Cha Nkonkilangi anako fanya kazi yeye.
Aidha kwa Upande wake John Binner naye alisema kuwa ,yeye ameona Mahakama Imetenda haki iliyopaswa kuitenda kwa kuwa Tangu amiliki Eneo hilo kihalali hajawahi kulipwa hata shilingi moja na Emmanuel , kama Walivyokubaliana.
No comments:
Post a Comment