Na Evarista Lucas
Singida
Nakumbuka vizuri
siku ambayo nilifurahi kupita kifani nilippopokea simu kutoka kwa rafiki
yangu kipenzi Halima “Jiandae best siku
ya Jumatano utaenda kutia saini mkataba.” Kabla
hata hajamaliza nilimuuliza mkataba wa nini tena swahiba? Bila kusita
akanambia “ Umepata ajira, unaenda kutia
saini mkataba baina yako na Klabu.”Kiukweli nilifurahi sana ukizingatia kwamba nilikaa nyumbani kwa muda mrefu toka nilipohitimu mafunzo yangu ya shahada ya awali ya mawasiliano ya umma katika Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino Mwanza. Si lengo langu haswaa kuwahabarisha haya yote lakini napenda mjue yafuatayo.
Mnamo mwaka 2011 mwezi siukumbuki vizuri; badhi ya Klabu (viongozi) za waandishi wa habari Tanzania zilisaini hati ya makubaliano kati yao na Muungano wa Klabu za waandishi wa Habari Tanzania(UTPC).
Kwa upande wa Klabu ya waandishi wa habari Singida(SINGPRESS0; mkataba huo ulisainiwa na aliyekuwa katibu mtendaji wa SINGPRESS wakati huo Bi Doris Meghji sambamba na Mwenyekiti Mch. Immanuel Barnaba
Hati hiyo ililenga kuzisaidia Klabu wanachama kwa kuwapatia vifaa, mafunzo,kulipia kodi ya pango kwa mwaka, kufunga mtandao wa intaneti, vocha za intaneti kwa mwaka na kulipia sehemu ya mshahara wa mratibu wa Klabu na pia mafunzo mbali mbali yenye lengo la kuwaongezea uwezo wa kitaaluma.
Ama kwa hakika wanachama wa
SINGPRESS wamenufaika vilivyo na mpango mkakati huu wa UTPC. Kwakuwa tangu mkataba huo kusainiwa tayari Klabu hiyo
imeshalipiwa fedha kwaajili ya kodi ya
pango la ofisi na pia wanachama wanaendelea kunufaika na mafunzo yanayotolewa
kwa awamu nne tofauti.
Mbali na hilo ;hivi karibuni
viongozi watatu (Mwenyekiti, Katibu Mtendaji na Mwekahazina) na wanachama
watatu wallipata fursa ya kufanya ziara ya kimafunzo katika Klabu ya waandishi
wa habari Kagera(KPC). Lengo kubwa la ziara hii ilikuwa ni kubadishana uzoefu wa kiutendaji.
Kwa upande mmoja naweza nikasema
ama kwa hakika tumevuna na kupata zaidi ya kile tulichokuwa tumekitaraji. Nasema hivyo kwa mantiki
zifuatazo; kwanza tumepata kujifunza jinsi wenzetu wa Kagera walivyonufaika
kupitia miradi waliyoomba ambapo tulidadisi namna walivyoomba na kufanikisha
kupata mikopo hiyo na pia kufahamu wafaddili waliofadhili miradi hiyo.
Mara tu baada ya kurejea kutoka
Kagera viongozi walijadili namna ambavyo wataweza kubuni miradi mbali mbali ya
kuiongezea kipato Klabu kwa kuomba uhisani kutoka taasisi na mashirika mbali
mbali.
“Mwenda bure si mkaa bure” Hatimae nasi tulipata fursa ya kutembelea
eneo la kihistoria ambapo vita vya Kagera mwaka 1978/1979
vilipigwa(Mutukula)mpakani mwa Tanzania na Uganda. Kwakuwa ilikuwa ni mara yetu ya kwanza kufika
mkoani Kagera; tulifurahi zaidi kwani tuliongeza elimu tuliyokuwa nayo aidha kwakusimuliwa
kuhusu vita vya Kagera ama kwa kusoma sasa tulijionea pia mabaki ya kanisa
lililopigwa mabomu na Nduli Idd Amin Dadaa.
Hatukuishia hapo tu; kwani ujio
wetu mkoani Kagera ulikuwa wa kipekee sit u kwa viongozi wa Klabu ya waandishi
wa habri Kagera; bali pia hata kwa baadhi ya waandishi na baadhi ya vituo vya
matangazo(Redio) kama ilivyokuwa kwa redio Kasbante fm.
“Tunawakaribisha sana hata kwa ziara binafsi au ya wote. Tumefarijika sana
na ujio wenu na nnafikiri kuwa Klabu zetu zitaleta mabadiliko makubwa katika
tasnia ya habari. Pia tunaomba kupata mwakilishi kutoka huko.” Alisisitiza
mtendaji mkuu wa redio kasbante Bwana Richard Leo.
Nae Afisa Masoko wa redio Kasbante
Bi Abella Kamala aliwaasa wanahabari kushirikiana haswa katika suala zima la
uhuru wa vyombo vya habari na pia kudumisha upendo na mshikamano miongoni mwa
waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment