Na, Daudi Nkuki
Singida
Ili ushirika upate hadhi
ya kujitegemea, hauna budi kuonyesha uwezo wa kukidhi vigezo vyote
vinavyotakiwa na kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (kkkt)dayosisi ya
kati.
Msaidizi Mteule wa
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kati Mchungaji Spriani Yohana Hilinti’amebainisha
hayo alipokuwa akizindua usharika mpya wa mazoezi wa msamaria mwema katika eneo
la Getwanus wilayani Hanang
Vigezo hivyo ni pamoja
na kuwa na uongozi kamili,akiwemo Mchungaji wa usharika ,jengo la kuabudia
,nyumba ya uchangaji na uwezo wa kimapato yasiyopungua shilingi 200,000/=kwa
mwezi kwa ajili ya kuhudumia usharika ,jimbo la Dayosisi na KKKT yenyewe.
Kwa mujibu wa historia
iliyotolwa kwa msaidizi mteule wa askofu,ibada ya kwanza ilifanyika April
21,1985 katika kijiji cha Getanuwas iliyohudhuriwa na wakisto wahamiaji 14 kutoka
sehemu mbali mbali nchini.
Mtaa ulifunguliwa rasmi
Julai 28,1985 na mchungaji Japhet Lalu kutoka ushirika wa Neema Mpipiti,ulioko
wilaya ya Singida Vijijini ,ambalo ni eneo la Dayosisi ya kati.
Kwa bahati mbaya kijiji
kilikumbwa na ghasia za vita vya kikabila ,baina ya wanyaturu na wabarabaig
,zilizowasambaratisha wahamiaji kukimbilia vijiji jirani
Baada ya vita kuisha
walirudi tena kuendelea na shughuli za kanisa,ikiwa ni pamoja na wazo la
kuanzisha ujenzi wa jengo la kuabudia mwaka 2000 hadi lilipokamilika mwaka 2010
Jengo hilo limgharimu
shs.40,000,000/= lililojengwa kwa nguvu za wakristo na michango yao wenyewe
bila kupata msaada wowote ,lina uwezo wa kuchukua watu 300 wakati mmoja.
Usharika wa msamaria
mwema umetokana na mitaa ya Getanuwas na samaria yenye jumla ya wakristo 680. kati
watu wazima 270 na watoto 410.pia ushirika umepata mchungaji mpya Japhet
Nakomolwa Kidindima
No comments:
Post a Comment