Na. Halima Jamal
Bagamoyo-pwani
Kwa mara nyingine kituo bora cha redio mkoani singida
(starndradiofm) kimejiongezea wigo wa uelewa kutokana na kupata mafunzo
yanayohusu maswala ya UKIMWI na jamii yaliyofanyika Bagamoyo mwanzoni mwa mwezi
huu.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na shirika la TACAIDS kupitia
shirika la GIZ yalishirikisha waandishi wa redio(prisenters) takribani 20
wakiwa wametoka sehemu mbalimbali za mikoa ya Tanzania.
Aidha lengo la kuwakutanisha waandishi hao ni pamoja na
kuwapa uelewa wa kutangaza vema dhana
inayohusu uhusiano na maradhi ya UKIMWI
katika jamii inayotuzunguka kwa vyombo vya habari hasa redio.
Katika mafunzo hayo yaliyoendeshwa na mkufunzi mwenye uzoefu
Dk Katanta Simwanza yalilenga hasa katika mfumo dume unaoendelea katika baadhi
ya familia tunazotoka kuwa mwanaume ndio kichwa cha nyumba katika mahitaji ya
kawaida
Katanta alisema kuwa familia nyingi maamuzi ya mwisho
yanatolewa na baba,ambapo si sawa kuwa hata mama katika familia anaweza kutoa
maamuzi ambayo yanaonekana kuwa sahihi.
''mfumo dume umegawanyika katika makundi matano,ambayo ni
majukumu,maamuzi,madaraka,ushiriki pamoja na umiliki wa rasilimali''alisema
Katanta.
Alifafanua kuwa katika majukumu ya mume na mke katika
familia yanatokana na wanaume wengi kukataza wake zao kufanya kazi na kuwaambia
wakae majumbani na kuwaletea wanachopata huko na kuwa mwanamke yule atakuwa
anamuogopa mume wake hata akimsikia ana wanawake hawezi kumuuliza kuogopa hatapewa
matumizi ya kila siku.
Alisema kuwa mwanamke anakuwa na jukumu la kulea watoto tu
na kwa upande wa madaraka idadi kubwa ya familia hupenda kumuona mwanamke kuwa
hafai kushika wadhifa wowote.
katika sehemu ya ushiriki Katanta lisema kuwa asilimia kubwa
wanaume hawakubali kushiriki katika kuwasindikiza wake zao cliniki pindi
wanapopata ujauzito.
Alisem katika suala ya umiliki wa rasilimali wanaume hupinga
kabisa wanawake kumiliki bali wao tu ndio wanaopaswa kumiliki ardhi hizo.
Katanta alisema kuwa katika hayo yote ndio hupelekea
maambukizi ya virusi vya UKIMWI kuendelea kusambaaa.
Hivyo basi waandishi wa habari hasa watangazaji wanatakiwa
waeleze jamii kuwa mfumo huo kuwa na mbaya na athari zake ni kuwa malezi na
makuzi kwa watoto wanaozaliwa mfumo huo unawapotosha bali kizazi hichi
kinachokuja kiwe na uelewa mzuri kuhusu hilo.
Mafunzo hayo ya Siku tatu yalioanza oct5 na kumalizika oct7
mwaka huu yaliwakilishwa na Halima Jamal kutoka standardradio Singida.
No comments:
Post a Comment