Na. Phesthow Sanga
Iramba, Singida
Chama Cha Mapinduzi {CCM} Wilaya ya Iramba Mkoani Singida,Kinajiandaa Kufanya Uchaguzi wake Mkuu wa ngazi ya Wilaya septemba 30- Mwaka huu kwa Nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya, pamoja na Nafasi ya {NEC}Taifa.
Katibu wa Wilaya ya Iramba Mathias Shidagisha amewataja wagombea kwa Nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya Ambao majina yao Yamerudishwa kutoka Halmashauri kuu ya ccm Taifa, ni pamoja na Charles Mkumbo Makala ,Moses Nalogwa Kitonka ,na Mwenyekiti ambaye muda wake Unaisha Wilson Nico Msengi .
Shidagisha amewataja Wagombea Wengine Wa nafasi ya Halmashauri kuu ya ccm Taifa {NEC} Kuwa ni Joseph Gerson Mlewa ,Michael Shankolo Kitundu, na Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Juma Hassan Killimbah.
Aidha Katibu huyo wa ccm Iramba Ameeleza kuwa Nafasi zingine 6 zinazo tarajiwa kufanyiwa Uchaguzi ni pamoja na Katibu Siasa na Uenezi Wilaya Nyenye Wagombea Watatu kati ya hao ni Daudi Amos Madelu ,Wazaeli Nahuva Maja,na Moses Nalogwa Kitonka.
Nafasi nyingine ni ya Katibu Uchumi na Fedha Wilaya nayo yenye Wagombea watatu Ambao ni Charles Mkumbo Makala ,Jen Henry Mtata, pamoja na Zacharia Elias Mkoma .
Aliwataja Wajumbe wengine wanaogombea Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya I ramba Yahya Nawanda ,Nafasi Inayogombaniwa na wagombea wapatao 14.
Nafasi nyingine ni Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya Ambayo Lina kundi la Wanawake lenye Wagombea Wawili kundi Lingine ni la Wazazi Wagombea Watano na kundi Jingine ni la Vijana Lenye Wagombea Watano pia .
Mathias Aliwataja Wajumbe Wengine Watano wanaogombea Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa ni Marimu Zabron Rajabu, Juma Swalehe Mhampa, Humphrey Timotheo Shango, Chanima Hamud Seifu,pamoja na Mathayo Shango Nguli.
Aidha wajumbe Wengine wa Halmashauri kuu ya Mkoa toka Iramba ni Rehema Mssa Mkasa ,Kinota Omary Khamis {JB},Timothy Wilson Lyanga,Jane Henry Matata, Elimamba Msafiri Lula, na SaidRamadhani Tyunu .
Aidha Katibu wa Wilaya Mathias, Amewaeleza Wagombea Pamoja na Wapiga kura kujihadhari na Tabia ya kutoa na kupokea Rushwa kwani wao Wameandaa VYombo vyote vya Usalama kupambana na Changamoto hiyo kwa kila Mtu atakaye jihusisha na Mtandao huo.
Hivyo Mtu yeyote asije kuulalamikia Uongozi kama Atapatikana na tatizo hilo la kutoa na kupokea Rushwa ,na Amewaomba Wajumbe wote ambao ni Wapiga Kura siku hiyo ya tarehe 30 kujitokeza kwa Wingi ili Waweze kumliza kazi hiyo iliyobakia ya kupata Viongozi wa Ngazi ya Wilaya.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment