Vitunguu ni miongoni mwa mazao ya biashara yanayolimwa mkoani Singida, wakulima na wafanya biashara kwa kipindi kirefu wamekuwa wakilima zao hili na kuliuza maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi, Hata hivyo bado zao hili linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa soko la uhakika pamoja na wakulima kukosa pembejeo; Serikali na mashirika yanawajibu wa kusaidia kupatikana kwa soko na matumizi mbadala ya vitunguu ama kwa kusindikwa na kupata soko nje ya nchi. Picha na. Doris Meghji
Na, Doris Meghji
Singida
Jumla ya
shilingi billion 85,216 zimepatikana kutokana na biashara ya zao la kitunguu
mkoani Singida katika kipindi cha fedha cha mwaka 2011/2012 ambapo tani 42,608
zilivuna na kuuzwa licha ya changamoto za maji na pembejeo zinawakabili wakulima
na wafanyabiashara wa zao la kitunguu
Kaimu katibu
tawala msaidizi huduma za uzalishaji mkoa wa Singida Bwana Charles Kidua ametoa
takwimu hizo ofisini kwake juu hali ya uzalishaji wa zao hilo la kitunguu kuwa
limekuwa likiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo kwa kipindi cha misimu mitatu cha
mwaka 2008/2009 tani 15,156 zilizalishwa,mwaka 2009/2010 tani 15,525 mwaka
2010/2011 tani 17 ,344 na mwaka 2011/2012 ya tani 42,608 zilizalishwa.
Aidha amesema
zao hilo la kitunguu likiwa ni moja ya mazao ya biashara mkoani hapo limeweza
kuajiri zaidi ya kaya 19,200 kutoka katika wilaya mbili za Iramba na Singida
katika vijiji vya Msange, maghojoa,kinyeto,puma na kinyangighi kwa wilaya
Singida huku wilaya ya Iramba ni vijiji vya Kaselya, Mwanga, Ilunda, Iguguno, Misigiri
na Dominiki
Zao la vitunguu
ambalo ni miongoni mwa mazao ya biashara katika mkoa wa Singida ambao pia
hulima alzeti na kuzalisha mafuta ya alizeti, vitunguu pekee huajiri zaidi ya
kaya 19,200 mkoani Singida
Hata hivyo
wafanyabiashara wa zao hilo la vitunguu mkoani Singida wameilalamikia hali ya
biashara ya zao hilo kuwa ya msimu kutokana na uzalishaji wake unaotegemea
msimu wa mvua pekee hivyo wameiomba serikali kuwachimbia visima vya maji na mabwawa
ya maji ili kuwa na upatikanaji wa maji ya uhakika na ilimo cha zao hilo kuwa
endelevu na sio la kutegemea msimu wa mvua pekee.
“tulikuwa
tunaomba msaada wa serikali kwa sababu wanasema sasa hivi ni kilimo kwanza
wangetuangalia labda na sisi kutusaidi kuchimbia maji na sisi ili tujiendeleze
kwa ajili ya kilimo cha kisasa kwa sababu kilimo cha msimu wa mvua ni kilimo
cha bahati nasibu. ”alisema makamu Mwenyekiti wa soko hilo na mkulima wa zao la
kitunguu Bwana Julius Majalo ambapo upatikanaji wa maji ya uhakiki
utandeleza biashara ya zao hilo kwa kutunza soko la vitunguu kuliko ilivyo sasa
kwa soko la zao hilo kuwa la mkoa wa singida pekee ukilinganisha na kipindi cha
msimu ambapo Kenya, Uganda,Rwanda,Burundi Kongo na sudani huwa wateja wao.
Naye mwenyekiti
wa madalali wa soko hilo Bwana Abrahaman Abdalah aliongelea suala la changamoto
ya pembejeo za kilimo hasa za zao hilo la kitunguu kutokuwa na maduka ya ruzuku
hasa mbolea kuuzwa kwa bei ya shilling 85,000/= “unaona mtu anajitahidi kulima
heka mbili tatu atahitaji labda mifuko kumi ya mbolea (10) ambayo ni shilling
laki nane na elfu hamsini (850,00/) tutalima kweli? tungeomba serikali ya mkoa
ya singida itusaidie ituwekee hata na sisi wakulima ituboreshee pembejeo kwa
kuwa na maduka ya ruzuku alisisitiza mwenyekiti huyo wa madalali sokoni hapo.
Katika kujibu
changamoto hizo katibu tawala msaidizi wa huduma za uzalishaji mkoani singida
Bwana Charles Kidua amesema katika kuendeleza kilimo serikali ya mkoa wa
singida huwashawishi wakulima wa kitunguu kuungana katika vikundi ili wafike
mahala wao wenyewe kuchimba visima."kuna baadhi ya maeneo tumewashawishi
vijana wakulima kuungana kwenye vikundi na wamechimba visima ikiwa pamoja na
kunua pambu ya kuvuta maji kwa ajili ya umwagiliaji na wengine
wamenufahaika kutokana na skimu za umwagiliaji kwa zao la mpunga. Serikali
haiwezi kumfikia mkulima mmoja mmoja."alisema bwana Kidua.
Aidha kwa suala
la pembejeo za kilimo amesema katika kipindi cha mwaka huu wa fedha jumla ya
tani 3 za mbolea yaminjingu kwa ajili ya kupandia na tani tano za mbloea
ya urea kwa ajili ya kukuzia zimetengewa bajeti ikwa ni pamoja na nusu
tani ya mbegu ya kitunguu ya aina ya Red Bombay katika mwaka huu wa fedha.
Kuhusu suala la
kuboresha mazingira ya soko hilo Kidua amesema halmashauri ya manispaa ya
singida imetenga bajeti ya kukarabati soko hilo katika kipindi hiki cha bajeti
kwa kuwajengea paa ikiwa ni pamoja na sakafu ili waweze kuhifadhi vizuri
vitunguu vyao.
1 comment:
uko juu nastori imetulia.
Post a Comment