Tuesday, March 5, 2013

WATUMA SALAAM SINGIDA NA UBUNIFU WA AINA YAKE

Baadhi ya kadi zilizoundwa na watuma salaam baada ya kukosa kadi harali za STANDARD RADIO katika maeneo yao

Ujio wa Standard Radio fm mkoani Singida, imekuwa kama ukombozi wa aina yake, viashiria vingingi vimethibitisha kuwa Standard radio imepokelewa na wanasingida na mikoa ya jirani kwa mikono miwili.

 

Vipindi vyake murua vimekuwa kivutio na kiunganishi muhimu kwa wananchi na viongozi wao, lakini pia kujenga na kuimarisha mahusiano baina ya jamii kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa na kijamii

 

Baadhi ya kipindi cha Salaam kwa njia ya kadi kuanza kila kona watu wamezisaka na pale walipozikosa waliamua kubuni namna ya kupata kadi hizo na kuzifikisha Studio ili salaam zao zisome.

 

Pichani hapo juu ni ubunifu uliofanywa na baadhi ya watuma salaam na wapenzi wa standard Radio mkoani Singida, Tabora, Dodoma na Manyara

Pichani, Ni kadi harali za standard radio zikiwa zimejazwa na wasikilizaji wa kipindi cha salaam

1 comment:

Anonymous said...

Ni kweli ni ubunifu wa aina yake.Ila nafikiri mngeteua mawakala wa kuuza kadi hasa kwenye maduka yalipo vyuoni naamni wanafunzi wengi wangezi chamgamkia kama njugu.
Ngairo
Buhanzo Enterprises
Dar es salaam.