Tuesday, March 12, 2013

TAARIFA YA HABARI MARCH 12, 2013


Source: SR/Neema J.

Ed: BM

Date: March 12, 2013.

 
SINGIDA

 

Mtu mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa  baada ya gari walilokuwa wakisafiria  kupinduka  baada ya kutokea hitilafu za kiufundi  na kusababisha ajali hiyo katika  kijiji cha  kisaki  tarafa ya mungu maji mkoani singida.

 

Kamanda wa polisi mkoani Singida ACP Linus Sinzumwa amesema ajali hiyo imetokea jana majira ya saa nne usiku katika barabara ya Singida kwenda Dodoma na kutaja namba ya usajili ya gari hilo kuwa ni gari namba C 6017 aina ya Nissan presage.

 

Kamanda Sinzumwa amesema chanzo cha ajali hiyo  ni kutokana na rock  hand  na driving  shaft ya gari hilo kukatika hivyo kusababisha ajali na kumtaja aliyefariki kuwa ni Abubakari Bukungukize ambaye ni mfanyabiashara wa Rwanda,  na aliyepata ajali ni  Vidal Ruse ambaye ni raia wa Sweden

 

Pia amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida na majeruhi bado anaendelea na matibabu na uchunguzi bado unaendelea kufanyika.

 

Amesema bado wanaendelea kuwasiliana na ndugu zao ili waje kuchua maiti na majeruhi huyo

 


Source: SR/

Ed: BM

Date: March 12, 2013.

 

KASULU

Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Kasulu Mkoani Kigoma Bw. Masud Kitowe ameuagiza uongozi wa kata ya shunguliba na kijiji cha malalo wilayani humo kuhakikisha mafundi waliopewa kazi ya kujenga nyumba ya mwalimu katika shule ya msingi malalo wanakamilisha ujenzi huo mara moja

 

Bw Kitowe ameyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha malalo wilayani kasulu baada ya kufanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata ya shunguliba sambamabamba na kufanya ukaguzi juu ya utekewlezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi.

 

Bw Kitowe amesema amepata taarifa kuwa mafundi waliopewa kazi ya kujenga nyumba hiyo wamesimama kuendelea na ujenzi kwa kile kinachodaiwa kuwa mafundi wamekwenda katika mashamba yao kulima. Amewaagiza viongozi hao kuhakikisha mafundi hao wanarejea na kumalizia ujenzi huo mara moja

 

Aidha Bw Kitowe amewataka viongozi hao kuhakikisha mafundi hao wanapatikana na kuendfelea na ujenzi wa nyumba hiyo na kama itashindikana basi mafundi hao warejeshe pesa walizopewa kwa ajili ya ujenzi huo na kuikabidhi kazi hiyo kwa mafundi wengine ili kukamilisha ujenzi wa nyumba hiyo ya mwalimu shuleni hapo


Source: SR/E. LYATUU

Ed: BM

Date: March 12, 2013.


SINGIDA

 

Wananchi Katika manispaa ya Singida wametakiwa kuwa  makini    na utupaji ovyo wa  taka  ili  kuweka   mji  safi  na  kuepukana   na  magonjwa  ya  mlipuko  mkoani   hapo

 

 

Bw. Seif  Swedy,  afisa  afya   na mazingira    wa   manispaa   amesema  hayo    wakati   akizungumza   na  standard    redio  ofisini  kwake.

 

 

Amesema  kuwa endapo wananchi wataonyesha  mwitikio kwa  kujituma kusafisha maeneo yao na kukusanya  taka  sehemu  moja,  hakutakuwa na  magonjwa ya   mlipuko kama  vile   kipindupindu    na   badala   yake mji  kuwa   safi na swala   la afya   kuwa   katika   usalama.

 

Hata hivyo  amesema chanzo  cha  taka  kuzagaa  ni kutokana   na  wananchi kutojali afya zao kutokana na hana  potofu  waliojiwekea  kwa kuamini suala la usafi linahusika na manispaa, hivyo  amewataka wananchi wawajibike  katika kuweka   mji  katika hali ya usafi.   

 

Bw  Seif  Swedy amewataka wananchi kuwa na mwamko wa  kujali mazingira kuwa katika hali  ya  usafi  na kila  mwananchi    kuwa mlinzi  wa mwenzake,  ili  kudhibiti tatizo la  utupaji   ovyo   wa  taka na kufuta dhana ya kutegemea manispaa   kuhusika  na  usafi   katika   mji  huo

 

Source: Tanzania Daima

Ed: BM

Date: March 12, 2013.

DAR ES SALAAM

Vituo vya televisheni vinavyomilikiwa na kampuni binafsi, viko hatarini kufungwa kutokana na mfumo wa matangazo wa digitali kuathiri upatikanaji wa matangazo.

Vituo vilivyopo kwenye hatari ya kufunga matangazo yao ni pamoja na ITV, Star TV, Clouds TV, DTV na vingine binafsi.

Taarifa za kufungwa kwa vituo hivyo, imetolewa jana na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini MOAT upande wa televisheni, wakati wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa MOAT, Bw. Reginald Mengi, amesema vituo hivyo viko hatarini kufungwa kwani idadi kubwa ya watumiaji wa televisheni imepungua kutokana na kukosa ving’amuzi na hivyo kuathiri upatikanaji wa matangazo.

Bw. Mengi amesema ili matangazo ya vituo vya televisheni yaendelee kupatikana, ameitaka serikali irejeshe matangazo ya analojia sambamba na digitali ili kuwapa nafasi watumiaji wa televisheni kujiandaa kuingia kwenye mfumo wa digitali.

Ameikosoa serikali kwa kuingiza matangazo ya mfumo wa digitali haraka bila kutoa muda wa kutosha kwa wananchi kujiandaa kwani haoni sababu ya Tanzania kuingia haraka kwenye mfumo huo.

Naye Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, anayemiliki kituo cha televisheni cha Clouds, amesema nusu ya matangazo kutoka kwa wateja wao yameondolewa baada ya matangazo yao kutowafikia watu wengi.

Kwa upande wake, Samuel Nyala, Mkurugenzi wa Sahara Media Group wamiliki wa kituo cha Star TV, amesema baadhi ya mikoa iliyoanza kurusha matangazo ya digitali, wamekwama kwani hakukuwa na maandalizi wakati mitambo ya analogia inazimwa.


Source: SR/Beatrice

Ed: BM

Date: March 12, 2013.

SINGIDA

Watu watano wakazi wa manispaa ya Singida, wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi, wakikabiliwa na shtaka la kuvunja na kuiba katika jengo la kampuni ya vinywaji ya Bonite, eneo la Mwenge mjini Singida.

Akisoma kesi hiyo mwendesha mashtaka, Bw. Mussa Chemu mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi, Bi. Telsefia Tesha, washtakiwa hao wamekana mashtaka dhidi yao.

Imeelezwa kuwa February 18 mwaka huu, majira ya usiku maeneo ya Mwenge ulifanyika uvunjaji huo na mali yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni ishirini na tatu Mali ya kampuni ya Bonite. 

Washtakiwa hao watano ni walinzi wa kampuni hiyo, ambao ni Zabron Ibrahim mkazi wa Puma Singida, Kautusi Francis mkazi wa Unyamikumbi Singida, Kassim Peter mkazi wa Misinko Singida, wengine ni Ladislaus Masini mkazi wa kibaoni Singida na Musa Gambuna mkazi wa kibaoni Singida.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 26 mwezi huu itakapotajwa tena, na upelelezi bado unaendelea kufanyika wakati washtakiwa wamerudishwa rumande. 


Source: SR/Matinde Nestory

Ed: BM

Date: March 12, 2013.

                                          

 MWANZA

Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka katika jiji la Mwanza Bw. Robert Masunya amewataka wananchi kujitokeza katika maadhimisho ya siku ya maji yatakayofanyika wiki hii

Wito huo umetolewa mapema hii leo wakati radio standard ilipokuwa ikifanya mazungumzo ofisini kwake

Bw.Masunya amesema kuwa maadhimisho hayo yatafanyika march 16 mwaka huu katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza ambapo kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji ni march 22 mwaka huu.

Meneja Uhusiano huyo amesema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu  katika siku ya maji ni MWAKA  WA  USHIRIKIANO  WA  MAJI  KIMATAIFA ambapo amewataka wananchi  kujitokeza katika maadhimisho hayo ambayo yanalenga katika kudumisha ushirikiano, upandaji miti katika vituo vya maji  pamoja na kutatua matatizo ya wananchi.

No comments: