Wednesday, November 28, 2012

WAANDISHI WA HABARI SOMENI SERA KWANZA

Baadhi ya waandishi wa habari wa Kigoma Press Club (Picha na. Prosper Kwigize)


Waandishi wa habari nchini Tanzania wamepewa changamoto ya kuandika na kuchambua sera mbalimbali za serikali na mashirika ya kiraia ili kuisaidia jamii kutafsiri sera hizo kulingana na maisha yao ya kila siku

rai hiyo imetolewa na mwalimu Robert Renatus Mkufunzi wa mafunzo ya uchambuzi wa sera na ufuatiliaji wa bajeti yanayofanyika kwa waandishi wa habari mkoani Kigoma kwa ufadhili wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania UTPC
Mwl. Robert Renatus, Mkufunzi na mwanachuo wa Chuo cha SAUT Mwanza


Mwalimu Renatus amebainisha kuwa, wandishi wasipojituma kuzijua na kuzichambua sera mbalimbali za taifa, itakuwa vigumu kwa watanzania kunufaika na habari nyingi zinazoandikwa bila kuwa na uchambuzi wa sera ya kile wanachoandika

kwa upande wao waandishi wa habari wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Kigoma wamekiri kuwepo kwa udhaifu mkubwa wa wanahabari kutoandika na kuchambua sera mbalimbali za maendeleo

Aidha wanahabari hao wamekiri pia kutozijua au kuzisoma sera mbalimbali za Tanzania

No comments: