Kijana unafaa kuwa kiongozi wetu, hata sisi wazee wa mkoa wa Singida tumeridhika na uamuzi wa Rais Kikwete kukupa nafasi hiyo, ulitumika vema katika nafasi uliyokuwa nayo awali, Sasa tunakutawaza kuwa mtemi wa Wanyiramba
Naibu katibu
Mkuu wa chama cha Mapinduzi { CCM}Tanzania Bara Mwigulu
Lameck Nchemba na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya
Taifa { NEC} Hivi juzi Alipokelewa
kama Mfalme katika
jimbo lake la
Iramba Magharibi kupongezwa Baada
ya kukwaa nyazifa
hizo mbili katika chaguzi
Zilizopita hivi karibuni
mjini Dodoma.
Mapokezi hayo ya kishujaa ni makubwa kuwahi kutokea, licha ya kuwa
mbunge wa jimbo la Iramba
magharibi, yalifanyika juzi Novemba
28 jumatano mwaka huu katika
Mji mdogo wa Ndago, sherehe ambazo
zilizofanyika ki-Mkoa,{Singida}.
Akihutubia Mkutano wa mamia ya wananchi
waliohudhuria katika sherehe hizo
za kumpongeza mhe Mwigulu Mbbunge wa
jimbo la
Mtera mjini Dodoma mhe. Livingston Vicent Joseph Lusinde
jina maarufu Msumari
wa moto aliwaambia wananchi kuwa jimbo la
Iramba magharibi, ”mmepata
Tunu tafadhali mwitumie ili
wilaya ya iramba pamoja na mkoa wa Singida
Uendelee kuheshimika kutokana
na kazi nzuri inayofanywa na kijana wenu Mwigulu.”alisema Lusinde
1 comment:
Ni kweli kwa wageni wa mji wa Ndago waweza kuona umati wa watu na kuamini kuwa mwigulu anapendwa na wananchi wa Iramba magh.Ila ukweli ni kwamba huyu kiongozi hapendwi na hatakiwi kabisa na wanajamii wa Ndago na Iramba nzima kwa ujumla.Hizo ni chaga za macho na hayo mapokezi yalijazwa na wageni toka wilaya jirani walioletwa kwa magari ya kukodi ili kuficha aibu ya mhe.Kiuhalisia wenyeji waliohudhuria mkutano huo hawazidi 03% wote.Na hii ni kwa sababu mhe.anatetea na kulinda maslahi ya ccm badala ya kutetea wapiga kura wake.Na suala hili linaweza kumfanya asirudi Bungeni katika uchaguzi wa 2015 kwani wananchi wengi sana wamehamia CHADEMA hasa baada ya makada wa ccm kudhaniwa kuwa walipanga njama yakuvuruga mkutano wa CHADEMA uliofanyika mji wa ndago Agusti 2012 na kusababisha mauaji ya mtu mmoja.Hili jambo liliudhi umati wa watu wa iramba magh.hadi leo.Hivyo mhe.anamtihani mgumu sana mwaka 2015 kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa 2014,madiwa ccm,ubunge na hata urais kwani kambi ya ccm iramba na singida kwa ujumla wake imeshaungua moto.
Post a Comment