Monday, December 3, 2012

MWIGULU NCHEMBA APOKELEWA KIFALME



Kijana unafaa kuwa kiongozi wetu, hata sisi wazee wa mkoa wa Singida tumeridhika na uamuzi wa Rais Kikwete kukupa nafasi hiyo, ulitumika vema katika nafasi uliyokuwa nayo awali, Sasa tunakutawaza kuwa mtemi wa Wanyiramba
 
Naibu katibu Mkuu wa chama  cha  Mapinduzi { CCM}Tanzania  Bara Mwigulu  Lameck  Nchemba  na Mjumbe wa Halmashauri  kuu ya  Taifa { NEC} Hivi  juzi Alipokelewa kama   Mfalme  katika  jimbo   lake   la Iramba  Magharibi kupongezwa  Baada  ya  kukwaa  nyazifa  hizo  mbili katika  chaguzi  Zilizopita  hivi  karibuni  mjini  Dodoma.

Mapokezi   hayo ya kishujaa ni makubwa kuwahi kutokea, licha  ya kuwa  mbunge wa jimbo la Iramba  magharibi, yalifanyika  juzi  Novemba  28 jumatano  mwaka  huu katika  Mji  mdogo  wa Ndago, sherehe  ambazo  zilizofanyika  ki-Mkoa,{Singida}.

Akihutubia  Mkutano wa mamia  ya wananchi  waliohudhuria katika sherehe  hizo za kumpongeza mhe Mwigulu  Mbbunge wa jimbo  la  Mtera mjini Dodoma mhe. Livingston Vicent Joseph  Lusinde  jina  maarufu  Msumari  wa moto  aliwaambia wananchi kuwa  jimbo la  Iramba magharibi, ”mmepata  Tunu  tafadhali mwitumie ili wilaya  ya  iramba pamoja na mkoa  wa Singida  Uendelee  kuheshimika  kutokana  na kazi  nzuri  inayofanywa na kijana  wenu Mwigulu.”alisema Lusinde

1 comment:

Unknown said...

Ni kweli kwa wageni wa mji wa Ndago waweza kuona umati wa watu na kuamini kuwa mwigulu anapendwa na wananchi wa Iramba magh.Ila ukweli ni kwamba huyu kiongozi hapendwi na hatakiwi kabisa na wanajamii wa Ndago na Iramba nzima kwa ujumla.Hizo ni chaga za macho na hayo mapokezi yalijazwa na wageni toka wilaya jirani walioletwa kwa magari ya kukodi ili kuficha aibu ya mhe.Kiuhalisia wenyeji waliohudhuria mkutano huo hawazidi 03% wote.Na hii ni kwa sababu mhe.anatetea na kulinda maslahi ya ccm badala ya kutetea wapiga kura wake.Na suala hili linaweza kumfanya asirudi Bungeni katika uchaguzi wa 2015 kwani wananchi wengi sana wamehamia CHADEMA hasa baada ya makada wa ccm kudhaniwa kuwa walipanga njama yakuvuruga mkutano wa CHADEMA uliofanyika mji wa ndago Agusti 2012 na kusababisha mauaji ya mtu mmoja.Hili jambo liliudhi umati wa watu wa iramba magh.hadi leo.Hivyo mhe.anamtihani mgumu sana mwaka 2015 kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa 2014,madiwa ccm,ubunge na hata urais kwani kambi ya ccm iramba na singida kwa ujumla wake imeshaungua moto.