JESHI la polisi mkoani
Sngida,linawashikilia watu 25 kwa tuhuma za kuteka gari la chuo kikuu cha
Sokoine (SUA) Morogoro na kisha kupora mali na fedha za watu waliokuwa wanasindikiza
maiti mwanafunzi wa chuo hicho kwenda mkoani Mara kwa ajili ya mazishi.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, Linus Sinzumwa, amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambalo limetokea jumapili desemba 9 eneo la Kisaki
katika wilaya ya Singida na kusema kwa sasa majina ya watuhumiwa hao
hayawezi kutangazwa hadharani kwa madai kuwa kitendo hicho kinaweza
kuathiri shughuli za upelelezi unaoendelea
Kamanda Sinzumwa amebainisha
kuwa, watekaji hao baada ya kuora mali za wasindikizaji hao, walivunja
jeneza na kasha kuupekua mwili wa marehemu Munchari Lyoba mwanafunzi wa
mwaka wa tatu katika chuo cha SUA,
Amelitaja gari lililotekwa
kuwa ni Toyota land cruiser lenye namba za usajili SU 37012 lililokuwa
likiendeshwa na Kalistus Mapulila, na kwamba mali zilizoporwa ni pamoja
na nguo za waathirika, kamera, kompyuta aina ya laptop na simu za mkononi
ambavyo jeshi la polisi limefanikiwa kuvikamata.
"Vitu vingine tulivyovikamata ni pamoja na vitambulisho vya kazi, charger
mbili za simu,kadi aina ya tembo kadi na shilingi 20,500 zizookotwa eneo la
tukio", alisema kamanda huyo na kuongeza kuwa mafanikio hayo
makubwa, yamechangiwa na ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi
Kamanda Sinzumwa ameongeza
kuwa watuhumiwa baada ya kugawana shilingi milioni 19.8 walizopora,
walianza kunywa pombe ovyo huku wakijitapa kuwa wana uwezo mzuri wa
kiuchumi",
|
No comments:
Post a Comment