Sunday, December 9, 2012

ARUSHA WAHITIMU MAFUNZO YA UJASILIAMALI

Mnara wa azimio la Arusha, lililolenga kujenga uzalendo na usawa wa kumiliki uchumi kwa watanzania, Mwl. Nyerere alitaka kila mtanzania awe mwaminifu, mwadilifu na anayelitumikia Taifa kwa dhati

Na. Beatrice Moses
Arusha Journalism Training College

Katibu Tawala wa wilaya ya Arusha Bw. Starnford Shayo awatunukia vyeti zaidi ya wahitimu 150 wa mafunzo ya ujasiriamali kutoka mikoa ya Arusha na Manyara, mahafali yaliyo fanyika mkoani Arusha yakiambatana na maonesho ya bidhaa mbalimbali yatakayo fikia kilele chake mnamo hii leo.

Akikabidhi vyeti hivyo kwa wahitimu hao Bw. Shayo amesema kuwa mapinduzi ya viwanda yanatokana na matumizi ya viwanda na kuhakikisha kuwa bidhaa zao zinatambulika Kitaifa na Kimataifa.

Aidha amesema kuwa serikali itahakikisha kuwa wajasiriamali wanasonga mbele kwa kuwataka kutengeneza bidhaa zao kwa mikono yao wenyewe pasipo kujali kiwango cha elimu walicho nacho.

Moja ya Mtaa wa Jiji jipya la Arusha, huu ni moja ya Miji ya Tanzania ambayo ni kitovu cha uchumi wa watanzania ingawa Raia wengi hawajatumia fursa zilizopo. Picha zote na Prosper Kwigize

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tanzania Business Creation Company (TBCC), Bwana Elibariki Mchau ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa wajasiriamali hao, ameiomba wizara ya Ardhi kuwapatia maeneo maalumu ya kufungua viwanda vya bidhaa ili kuweza kufanya shughuli zao na kuipatia fursa serikali kukusanya kodi kwa urahisi zaidi.

Bw. Mchau ameongeza kuwa hadi kufikia mwaka 2015 wajasiriamali hao watakuwa na uwezo wa kutengeneza nafasi za ajira kwa watanzania walio wengi, na hivyo kuipunguzia serikali mzigo wa ukosefu wa nafasi za ajira.

wajasiriamali hao wana uwezo wa kutengeneza bidhaa mbalimbali zikiwemo sabuni za miche, sabuni ya unga pamoja na sabuni za maji kwa ajili ya kusafisha maeneo mbalimbali kama vile injini za magari, mochuari, mabuchani na sehemu ambazo zina uchafu sugu.

No comments: