Thursday, December 27, 2012

TPSC SINGIDA NA MKAKATI WA MAENDELEO


Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma cha mkoani Singida Bw. Levi Kulamwa (pichani) ametangaza kuwasaidia wahitimu wa Kidato cha nne kote nchini kupata fursa ya kujiendeleza kielimu kwa kuwapatia nafasi za masomo na kozi mbalimbali katika chuo hicho

hata hivyo ametoa changamoto kuwa wanaostahili kudahiliwa na huo hicho ni wale wenye ufaulu mzuri pamoja na waliopata angalau alama D katika mitihani yao ya kumaliza kidato cha nne


Jengo la utawala la CHuo cha utumishi wa Umma Singida, Licha ya kuwa tawi changa mkoani humo, kimefanikiwa kudahili wanachuo zaidi ya elfu moja ambao wanapata mafunzo ya kozi mbalimbali. Matarajio ya Chuo hicho ni kuwawezesha vijana wa Tanzania kuingia katika ushindani wa soko huria la ajira ndani na nje ya Tanzania (anasema Bw. Kulemwa, mkuu wa chuo hicho)

No comments: