Wednesday, December 12, 2012

ELIMU HAINA MWISHO

Watumishi wa Standard radio wakiwa katika mafunzo ya kitaaluma yaliyoandaliwa na utawala wa kampuni ya Standard Voice Limited
Na Edilituda Chami
Katika kuhakikisha tasnia ya habari  inasonga mbele waandishi wa habari wa standard radio fm  iliyopo mkoani Singida wamepatiwa mafunzo ya mrejesho wa uandishi wa habari kama ishara ya kuwaongoza katika shughuli zao za kila siku
Mwezeshaji wa mafunzo hayo  Bw. Boniface Mpagape amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kujiandaa zaidi kwa ajili ya ufanisi na ubora katika tasnia ya habari na kueleza kuwa ni vyema kila mtu kutambua kuwa elimu haina mwisho

Aidha waandishi hao wametakiwa kuwa makini katika uandaaji wa habari na kuepuka habari zisizo sahihi na zinazoleta mtafaruku na upotoshaji katika jamii kwani kwa kufanya hivyo jamii itajenga fikra mbaya kwa waandishi wa habari
Naye Mratibu mradi wa Standard Radio Bw. Prosper Kwigize amewapa mbinu  mbalimbali ambazo mwandishi wa habari anaweza kutumia ili habari yake iwe na  mvuto, faida na yenye kuleta maendeleo na mabadiliko katika jamii

Waandishi hao wameushukuru uongozi wa standard radio kwa kubuni mtindo huo wa kutoa mafunzo kwani wameweza kujifunza mambo ambayo ni mageni kwao na ya kuelimisha na kuamini msemo usemao ‘ elimu haina mwisho’

No comments: