Tela la lori la mafuta ya petroli lilolokuwa likitoka Dar es salaam kwenda
wilayani Ngara mkoani Kagera limeanguka alfajiri 28/12/2012 katika eneo la kisaki
manispaa ya Singida na kunusurika kuungua
Akielezea chanzo cha ajali hiyo dereva wa gari hilo Bw.
Abdulrahman Shaban amesema lori alIlokuwa akiendesha aina ya Mercedes Benz lenye namba za usajili T 776
ARL lenye tela namba T 123 ASQ, alikutana
na lori jingine lililokuwa limewasha taa kali
zilizomsababisha kutoona mbele na kuacha njia kabla ya kuanguka
Amemtaja mmiliki wa
lori hilo kuwa ni Bw. Suleiman Hilal
Mohamed maarufu kwa jina la Medi mkazi wa Kabanga wilaya ya Ngara.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida Bw. Linus Sinzumwa
amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba raia wamethibitiwa vyema kuzuia
uporaji wa mafuta ambao ungeweza kusababisha mlipuko wa moto na vifo.
Kikosi cha askari polisi kwa kushirikiana na kikosi
cha zimamoto na uokoaji mkoani Singida wamefanikiwa kuzuia wananchi waliokuwa
wakitaka kuchota mafuta ya petrol yaliyomwagika. Mrakibu mwandamizi wa kikosi cha zimamoto na uokoaji mkoani Singida Bw. Kevin Mapunda, amesema raia wengi baada ya kupata taarifa za kutokea kwa ajali hiyo, walikusanyika kwa lengo la kujinufaisha kwa kupora mafuta pasipo kuhofia kutokea ajali nyingine ya mlipuko wa moto.
Tukio la kupinduka kwa lori la mafuta liliwahi kusababisha
watu 44 kujeruhiwa vibaya kwa moto wakati wakipora mafuta katika wilaya ya Manyoni mkoani Singida miaka ya nyuma.
No comments:
Post a Comment