Wednesday, December 5, 2012

TCRA KUZIMA MITAMBO YA ANALOGIA

Na. Prosper Kwigize
Dares Salaam
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania imesisitiza kuwa itazima mitambo ya analogia ifikapo December 31 mwaka huu na kusisitiza watanzania kuanza kununua ving’amuzi vya digitali mapema
Tamko hilo limetolewa leo na mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Profesa John Nkoma wakati akifungua semina ya wadau wa utandazaji Tanzania inayoendelea jijini Dar es Salaam
Hata hivyo profesa Nkoma amekiri kuwa mfumo huo wa matangazo haujasambaa nchi nzima na kuitaja mikoa ambayo iko tayari kwa mfumo wa diditali kuwa ni Dar es salaam, Arusha, Mwanza, Dodoma na Mbeya
Akitaja faida za mfumo huo mpya na sababu za Tanzania kuwahi kujiunga nao amesisitiza kuwa, digitali inalahisisha urushaji wa mawimbi ya sauti na picha kwa ubora zaidi na inapunguza gharama kwa watangazaji
Prof. Nkoma (kulia) akifuatilia maoni ya wadau wa warsha hiyo
 
Aidha prof. Nkoma amebainisha kuwa, lengo la kuwa kufanya hivyo pia ni pamoja na kuzuia Tanzania kuwa soko na dampo la vifaa vya analogia ambavyo nchi nyingi zimeacha kuvitumia
Dr. Ayub Lioba mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam  idara ya habari na mawasiliano ya umma (TSJ) akichangia mada kuhusu mfumo wa matangazo kwa njia ya Gigitali Tanzania
 
Zaidi ya wadau miamoja kutoa vituo vya Radio na television (runinga) Tanzania wameshiriki warsha hiyo ambayoni maandalizi ya mkutano kuu wa TCRA wa mwaka 2012 utakaofanyika kesho katika hoteli ya Kunduchi Beach
Mr. Paschal Mwalyenga, fundi mitambo wa Radio Kwizera Ngara akisikiliza kwa umakini mada ya mabadiliko ya mfumo wa analogia kwenda Digitali
 

No comments: