Na. Elizabeth Martine
WAFANYAKAZI WA STANDARD RADIO FM WAMEKABIDHI MCHANGO WA RAMBIRAMBI KWA MFANYAKAZI MWENZAO BW. BONIFACE MPAGAPE KWA KUFIWA NA NDUGU YAKE
BW. MPAGAPE AMBAYE NI MHARIRI WA STANDARD RADIO ALIFIWA NA KAKA YAKE Bw. MBUTA MIRANDO, AMBAYE AMEWAHI KUWA KATIBU MWENYEZI WA TANU (T), MKUU WA WILAYA WA KWANZA WA WILAYA YA GEITA NA NGARA
MAREHEMU MIRANDO PIA ALIWAHI KUWA KAIMU BALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA KABLA YA KUTEULIWA NA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS NYERERE KUWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI CANADA HADI ALIPOSTAAFU MWAKA 1970, KABLA YA KIFO CHAKE KILICHOTOKEA December MOSI 2012 JIJINI MWANZA ALIKUWA AKIFANYA SHUGHULI BINAFSI.
WAFANYAKAZI WA HAO WAMEMKABIDHI KIASI CHA SHILINGI 32,000/= IKIWA NI ISHARA KUONESHA KUGUSWA NA TUKIO LA MWENZAO SAMBAMBA NA KUIMARISHA MAHUSIANO MIONGONI MWAO.
AKIKABIDHI FEDHA HIZO MRATIBU WA MRADI WA STANDARD RADIO BW. PROSPER KWIGIZE KWA NDUGU BONIFACE MPAGAPE AMESEMA KUWA MCHANGO HUO UMETOLEWA NA WAFANYAKAZI HAO IKIWA NI ISHARA YA UPENDO, UMOJA NA USHIRIKIANO MIONGONI MWAO.
KWA UPANDE WAKE BW. MPAGAPE AKIPOKEA MCHANGO HUO, AMEWASHUKURU WAFANYAKAZI WOTE WA MAKAMPUNI YA STANDARD VOICE LIMITED NA BUHANZO ENTERPRISES NA KUWAOMBA WAWE NA MOYO WA USHIRIKIANO HUO KWA WENGINE.
MAMAREHEMU MIRANDO AMEACHA MJANE MMOJA, WATOTO WATANO, WAJUKUU KUMIA NA WATANO NA KITUKUU KIMOJA, AIDHA AMEZIKWA KATIKA MAKABURI YA KIRUMBA JIJINI MWANZA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 78.
No comments:
Post a Comment