Mkuu wa wilaya ya SIngida akipanda mti katika siku maalumu ya upandaji miti katika manspaa ya Singida katika kampeni maalumu ya kutokomeza jangwa. picha na Ediltruda Chami
Na. Edilitruda Chami na Elizabeth Martin.
Mkuu wa wilaya ya
Singida Bi. Queen Mlozi amesema
kuwa ni vyema kila mwananchi wa mkoa wa Singida kushiriki katika shughuli za
upandaji miti ili kuondokana na hali ya ukame unaosababisha hali ngumu ya
maisha mkoani Singida.
Wito huo ameutoa leo katika
Uzinduzi wa awamu ya pili wa kampeni ya vita dhidi ya jangwa na miaka hamsini
na moja ya uhuru katika kijiji cha Kitope kata ya Mandewa mkoani Singida.
Katika uzinduzi huo jumla ya miti 400 aina ya miti maji
inayotoa sabuni na mbao, imepandwa ikiwa kama ishara ya mwendelezo wa
tukio hilo ambapo miti hiyo huchanua kila baada ya miaka mitatu
Katika hotuba yake Bi. Mlozi amewataka wananchi kushiriki
katika upandaji wa miti pamoja na ufugaji wa nyuki, sambamba na kuwa mstari wa
mbele katika kuzuia uharibifu wa mazingira kwani wananchi wa mkoa wa Singida wanaongoza
kwa kuchoma mkaa na kusafirisha nje ya mkoa na kwamba atakayekamatwa akichoma
mkaa sheria itachukua mkondo wake.
Hata hivyo wananchi waliohudhuria katika uzinduzi huo
wameshukuru uongozi wa manispaa ya Singida kwa mkakati huo wa upandaji miti
walioanzisha kwani wanaamini kwa kufanya hivyo, Singida itaonekana kjani na
sivyo kama watu walivyojijengea kuwa Singida ni kame na kuwa mstari wa mbele
kutimiza kauli mbiu ya ” kata mti panda mti”.
Kampeni hiyo imezinduliwa chini ya mradi wa taasisi binafsi
ijulikanayo kwa jina la Anti Desert. Kampeni ya upandaji miti ngazi ya Manispaa
ya Singida inatarajiwa kufanyika tarehe 4 Januari mwaka 2013, katika shule ya
msingi Unyinga mjini Singida. Awamu ya
kwanza ya kampeni hiyo ilifanyika mwaka 2006.
No comments:
Post a Comment