Tuesday, December 11, 2012

STANDARD RADIO YATOA MAFUNZO KWA WATUMISHI WAKE

Waandishi wa habari wa Standard Radio FM wakifuatilia kwa umakini mafunzo ya ufahamu na utambuzi wa malengo, dira, dhima na maudhui ya Radio hiyo iliyoko mjini Singida ambayo katika kipindi kifupi kijacho itaanza kurusha matangazo yake rasimi baada ya mchakato wa ufungaji wa mitambo kukamilika wiki ijayo. kutoka kushoto ni Hadija Mahamba, Boniface Mpagape, Eufrasia Mathias na Elizabeth Martine. Picha zote na. Moses Athony John
Na. Elizabeth Martine
WAFANYAKAZI WA STANDARD RADIO WAMEFANYA MAFUNZO IKIWA NI MCHAKATO WA MAANDALIZI YA URUSHAJI WA MATANGAZO RASMI UNAOTARAJIWA KUANZA RASMI JANUARI 2013.
AKIZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA STANDARD RADIO FM KITUONI HAPO MRATIBU WA STANDARD RADIO BW. PROSPER KWIGIZ KATIKA SEMINA HIYO DESEMBA 11, 2012 AMETAJA  MALENGO MAKUBWA YA RADIO NI KUHABARISHA, KUELIMISHA NA KUBURUDISHA JAMII YA MKOA WA SINGIDA NA SEHEMU JIRANI AMBAZO MATANGAZO YATAZIFIKIA.
BW. KWIGIZE AMESISITIZA KUWA MALENGO HASA YA KUANZISHWA KITUO HICHO CHA RADIO KUWA NI KUWAPA FURSA WAKAZI WA SINGIDA KUTOA KERO ZAO ILI ZIWEZE KUSIKIKA KWANI NI MUDA MREFU HAWAKUSIKIKA.

PICHA. Bw. Prosper Kwigize akitoa semina kwa watumishi wa standard Radio kuhusu sera, dira na mtazamo wa Standard radio FM mjini Singida

AMESEMA STANDARD RADIO FM ITASAIDIA PIA WAKULIMA WA MKOA WA SINGIDA NA MAENEO MENGINE YA JIRANI KUJIFUNZA KUHUSU UJASIRIAMALI, KILIMO PAMOJA NA KUJUA WAPI MASOKO YANAPATIKANA ILI WAONDOKANE NA UMASIKINI
AIDHA BW. KWIGIZE AMEWATAKA WAFANYAKAZI WOTE KUTAMBUA KUWA WAAJIRI WAO NI WASIKIKLIZAJI WA STANDARD AMBAO KUPITIA KWAO MAISHA BORA KWA WAANDISHI NA WANANCHI WENYEWE YATAPATIKANA

STANDARD RADIO FM IMETOKANA NA STANDARD VOICE LIMITED CHINI YA UANGALIZI WA KAMPUNI YA BUHANZO INTERPRISES KWA LENGO LA KUSIMAMIA KITUO
KATIKA MAFUNZO HAYO WAFANYAKAZI WOTE WAPATAO KUMI WAMEJIFUNZA JUU YA DHIMA, DIRA NA MUONO WA RADIO PAMOJA NA MAUDHUI NA MALENGO YA UANZISHWAJI WA KITUO HICHO
HATA HIVYO KATIKA SEMINA HIYO WAFANYAKAZI WA KITUO HICHO WAMETOA MAONI MBALIMBALI IKIWA NI KUWATAKA KILA MMOJA KUONYESHA USHIRIKIANO NA KUJITUMA ILI KUWEZA KUFIKIA MALENGO NA KULETA MAENDELEO KATIKA JAMII NA TAIFA KWA UJUMLA.

Waandishi wa SR fm Boniface Mpagape na Khadija Mahamba wakifurahia baada ya kutaarifiwa kuwa mitambo iliyokuwa imekwama nchini Afrika kusini imewasili tayari kwa kukamirisha shughuli za kufunga mitambo na kuanza kwa matangazo
Dreva wa SR fm Bw. Noel Exavery akipokea simu nje ya ofisi, akitaarifiwa kujiandaa kuipokea mitambo mipya ya radio hiyo 

No comments: